Wasafi.com yavuka border! Diamond azuru Uhispania kukutana na waekezaji wanaotaka kuekeza wasafi.com

Diamond Platnumz alizindua tovuti yake ya kuuzia muziki unaoitwa Wasafidotcom. Super star huyu amekuwa akifanya mikutano ofisini kwake na wasanii mbalimbali, kuzungumza namna ya kufanya nao kazi kwenye mradi huo. Tayari amekutana na wasanii kama Ben Pol, Barnaba, Chege na hata Willy Paul Kutoka Kenya.

Msanii huyo wa muziki ya injili – Willy Paul alikubaliana na Diamond kuweka muziki wake mpya na Alaine ‘I Do’ kwa tovuti Wasafi.com.

download latest music    
Diamond and Willy Paul

Jana Diamond alisafiri kuelekea Uhispania kufanya mazungumzo na waekezaji wanaotaka kuekeza wasafi.com.

Hitmaker huyo wa Marry You alisema kuwa atafanya kikao kifupi na waekezaji kabla ya kuelekea nchini Oman kufanya show yake.

“Kikao kifupi Nchini Spain kuhusu @wasafidotcom kabla ya show yangu mjini Muscat, Oman ijumaa hii… wadau natamani niwadokeze walau kidogo jinsi tasnia yetu iendapo huu mwaka…?? tafadhali msiache kuniombea?” Diamond aliandika kwenye caption ya picha yake.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere