Yamoto Band yatoa wimbo mpya baada ya kuzuka minong’ono mitaani juu ya ukimya wao

Ukimya wa Yamoto Band ulichangia kuzuka kwa uvumi kuwa kundi hilo limesambaratika. Kiongozi wa Mkubwa na Wanawe Said Fella alisisitiza kuwa bado Yamoto Band wako pamoja ingawa kila mmoja anaishi kivyake.

“Maneno yalikuwa mengi juu ya Yamoto Band yetu lakini sisi tulikuwa kimya na mengi yalisemwa na leo tumeleta wimbo mpya unaitwa Basi,” Mkubwa Fella aliambia Clouds FM.

download latest music    

Ukweli wa matamshi yake ulidhihirika pale ambapo Diamond alitangaza kuwa Yamoto Band wametoa wimbo mpya.

“Brand New Hit from @Yamoto_Band #BASI it’s now Exclusively Available on @wasafidotcom (Moja ya ngoma nilokuwa nikiisubiria kwa hamu toka yamoto band sasa imetoka inaitwa #BASI na inapatikana ndani ya @wasafidotcom Wadau tuwatie Moyo vijana wetu kwa kuinunua kwa mia 300 tu….Maana, Huu ndio Muda wa kumuunga mkono Msanii Umpendae…” Diamond aliandika kwa Instagram.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere