Nguzo Za Kufanikiwa Katika Elimu Na Biashara

Hakuna ambae hataki kusogea kutoka pale alpo na kufika sehemu nzuri zaidi,mafanikio yanamfanyan mtu anakuwa jasiri na kuwa na amani ya kile anachokifanya, ikitokea mtu anafanya kitu lakini hakuna mafanikio ujikuta anakta tamaaa na kuacha kabisa kuendelea na jambo fulani.sio kila mwenye majumba, magari na fedha nyingi basi huyo amefanikiwa.kuna watu wanakuwa na hivyo vyote kupitia njia ambazo sio halali kabisa.mafanikio ni vile mtu ameweza kuanza toka chini na kufikia hali hiyo.

kwaio ili kufanikiwa ni azima kuwa na nguzo  zifuatazo;

download latest music    

1.kupanga

siku zote mipango ndio inatoa majukumu ya  kufanya. kwa mfano kama leo ujapanga ni kitu gani unataka kufanya kesho yake unaweza kujikuta kesho kuanzia asubui umelala au unazunguka tu siku nzima bila kuwa na sababu.katika kupanga ni lazima uwe na maono ya kile unachotaka kufanikiwa kuwa nacho ndani ya muda fulani.

2.Kupenda kufanya unachokifanya.

Hapa tunazungumzia kitu kinaitwa Passion.Hii ni vile unaweza kujitoa na kujituma zaidi ilikupata yale mafanikio uliokuwa umeyapanga,jitahidi kukipenda kile unachokifanya lakini kama ya kukipenda wakati unakicgahua hakikisha kinatoka ndani ya moyo wako.Kwa mfano wapo wanaolazimika kusoma kozi fulani kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao basi jitahidi kupoenda hicho kitu na kama unaona haitawezekana ni bora kuacha.Kwa mwanafunzi anaesomea sayansi, endapo atakuwa anapenda sayansi basi atakuwa anajitaidi kupata  alama A kila siku kwa sbabu ni kitu anachokipenda.

3.Kuwa mwenye kujiamini

Siku zote ukishakuwa mwenye kujiamini unakuwa na moyo wa kuchukua hatua za kila unachotaka kufanya.Hata kama kuna watu wanakufanya ukate tamaa ukishajiamini wala hauna haja ya kusikilza nani anasema nini.

4.Kuvumilia

Hakuna kazi ,biashara au elimu ambayo haina makwazo na changamoto, hakuna kitu rahisi  Duniani lakini uvumilivu ndio utakao kufanya wewe uweze kufanikiwa katika kila unachotaka kuweka mafanikio.Kuna muda utaona kabisa mambo yanakuwa magumu, hapo ndipo unatakiwa kuonyesha ni jinsi gani ulikuwa tayari kufanikwa kwa kuonyesha uvumilivu wako katika hilo.

5.Kuwa na mpango mbadala

Sio kila utakachoamua kufanya kwa muda huo kinaweza kufanikiwa, hapana !! lakini kuna muda unahitaji kuwa na njia mbadala ya kufanya baada ya kile ulichokifanya kwanza kushindwa.Wapo ambao wanapoona njia ya kwanza imeshindikana basi na wao wanaachia hapohapo.kuwa na njia mbadala ya ile ya kwanza ili kuweza kufika malengo.

6.Fanya vitu  kwa vipaumbele.

Katika kufanya jambo ni lazima ujue lipi ni la muhimu zaidi kuliko lingine, kuwa na akili ya kuchambua mambo unayotaka kufanya na kujua kipi kinatakiwa lianze na lipi kinafuata baada ya hicho.Katika mipango yako siku zote jua kipi ni muhimu zaidi cha kwanza na kinachofuata na kinachofuata na ujue sababu ya kufanya jambo fulani kuwa ni la muhimu zaidi kuliko lingine.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.