Tabia Zinazoweza kumfanya Mwanamke Kukosa Kuwa Na Mahusiano

Image: (C)Daniel Butcher 2007

Kuna baadhi ya wataalamu wa mahusiano wanasema kuwa kuna baadhi ya vitabia wanaweake wamekuwa  navyo ambavyo wanaviona ni vya kawaida na wakati mwingine wanaona ni haki yao kabisa kuvifanya lakini ukweli ni kwamba tabia hizo zinaweza kmkimbiza mwanaume anaetaka kuanza mahusiano na wewe akaacha kukuelezea hisia zake.

1.Endapo mwanamke atapigiwa kwa namba mpya, basi anauliza namba yangu umepata wapi, usiponiambia nani amekupa basi usianipie.hii uwafanya wanaume wengi kukata tama, mtu mpaka ametafuta namba yako basi ujue ana shida na wewe, ni bora ukamsikiliza kwanza nini anataka.

download latest music    

2.Mwanamke unaingia kwenye chombo cha usafiri ambacho ni public, unakaa kwenye seat ambayo umekuta mingine amekaa, unachukua earphones unawela masikioni bila hata kusalimia na kujifanya utaki kusemeshwa, hii pia uwakatisha tamaa wanaume.

3.Mwanamke amekutana na mtu njiani , anakusalimia unajibu akikuongelesha tena unachuna, ikibidi unajibu vibaya.unashindwa kutambua kuwa mahusiano yoyote uanza na salamu.

4.Mwanamke unaenda nyumbani kwa mwanaume, unamkuta yeye anakula ugali, unakataaa ugali unaagiza chipsi au unajibu kuwa kabisa huwezi kula ugali,Dada ndoa yako iko mbali.

5.Mwanamke anaanza uhusiano na mwanaume, siku mbili u tatu tu anaanza kumuomba ela na kumuorodhoshea matatizo ya familia yake nzima bila hata kujua mwenzie yukoje. Wanaume wengine watakuogopa ingawa wao watakaokuvumila kwa muda.

6.Wanawake wengine wamekuwa na tabia ya kuchart na wanaume huku reply zao zikiwa ni p,k, na vifupi vingi visivyoeleweka, sio kila mmoja anaelewa lugha ya mtaani uliyokulia wewe, unapokutana na mtu siku za mwanzo inabidi kumjua na kujua vituanapenda kuongea.wapo wengi uhusiha maongezi yao na lugha za matusi.

Nyingi ya tabia hizi huwa ni z mazoea sana kwa wanawake, na anaweza kuwa anajiona yuko sawa kabisa anapokuwa anafanya bila kujua kuwa swala la mahusiano pia ujengwa na tabia.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.