Baba Kanumba Atuma Ujumbe Mzito Kwa Lulu

Baba mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Charles Kanumba ‘Baba Kanumba’ ameibuka na kudai kuwa anamsaka Elizabeth Michael ‘Lulu’ ili ampe ujumbe wake.

Siku chache Baada ya Lulu kumaliza kifungo chake, Baba Kanumba amesema anamsaka Lulu ili aweze kumpa nasaha zake kama baba pamoja na ujumbe aliopewa na babu wa Kanumba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi, Baba Kanumba alifunguka kuwa siku chache kabla Lulu hajamaliza kifungo, alitokewa na babu wa Kanumba yaani baba yake mzazi ambaye alifariki wakati mwanaye Kanumba anazaliwa na kupewa jina lake.

Babu wa Kanumba alinitokea na kuniambia nimkumbushe Lulu atekeleze mambo ya kimila ambayo nimewahi kumwambia tena ya kwenda kaburini kwa Kanumba na kufanya usafi na kumuombea na hapo atakuwa ameondokana na kile kivuli cha marehemu.

Wakati Lulu anafanya hayo anatakiwa awepo ndugu wa upande wa ukoo wa Kanumba ili kushuhudia na akimaliza hayo atakuwa yupo salama na hatapata mikosi tena kwenye maisha yake na kile kivuli cha Kanumba kitakuwa kimemuondoka lakini vinginevyo atapata taabu”.

Lakini Mzee Kanumba alisema hamlazimishi Lulu kufanya hayo mambo na pia amekiri kuwa hana kinyongo na Lulu hata kidogo na kumtakia kila la kheri maishani.

Sina kinyongo na Lulu, nimefurahi sana yeye kumaliza kifungo na ninamuombea mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake, ninahitaji na ninamsaka sana kwa udi na uvumba maana nina mengi ya kumwambia kama mwanangu”.

 

Baba Kanumba Hakuridhika Na Hukumu Ya Lulu

Wakati watu wengine wakilalamika na wazazi wa msanii Lulu Michael hata kuzimia na kushindwa kutembea kutokana na hukumu aliopewa msanii Lulu Michael ya kutumikia kifungo kwa miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua marehemu Steven Kanumba bila kukusudia , baba mzazi wa marehemu Kanumba amefunguka na kusema kuwa hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama ni sawa na mtu alieua kuku tu.

Akiongea kwa njia ya simu moja kwa moja kutoka mkoani Shinyanga anapoishi mzee huyo na mwandishi wa Global publisher, baba Kanumba aliulizwa anasemaje maoni yake kuhusu hukumu aliyopewa Lulu baaada ya kukutwa na hatia ya kumuua mwanae bila kukusudia na alijibu kuwa

Kwa upande wangu kwanini  hukumu hii imekuwa  ndogo sana, na haijanifurahisha hata kidogo, hata kama mtu aliua kwa kutokukusudia  lakini mahakama imetoa kifungo cha miaka miwili kweli kama mtu kaua kuku.-Alifunguka mzazi huyo

Hata hivyo alipoulizwa kama angefurahi ni miaka mingapi ambayo alitegemea Lulu angepewa mzazi huyo alisema kuwa,

nilitegemea kuwa mahakama ingetoa hata kuanzia miaka mitano,sita,saba na kuendelea.

Hata hiVyo kuhusu yeye kutokuwa anaonekana mahakamani, baba mzazi wa Kanumba alisema kuwa alishindwa kuja ili kukwepa gharama na ndio maana alimuachia mama yake aweze kufatilia swala hilo hata hivyo anaona ingekuwa ni upotevu wa pesa maana hata hiyo hukumu yenyewe sio ya msingi sana.

Sikuja huku nilimwachia mke wangu aendelee na kesi  hiyo kutokana na kupunguza  sizizo na msing na ndo hivyo hukumu yenyewe  ni miaka miwili tu kama mtu kaua kuku.si ningepoteza muda wangu tu hapo na hukumu yenyewe haikunifurahisha  kulingana na mazingira ya kifo cha mtoto wangu .-Aliongezea Baba Kanumba

Lulu Michael alimuua Kanumba bila kukusudia miaka kama mitano iliyopita na baada ya kesi yake kushughulikiwa kwa muda mrefu ameweza kuukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kitu ambacho kiliibua pia hisia za watu wengi wanaompenda Lulu na  watu wengi kuonekana na majonzi kutokana na hukumu hiyo huku kila mmoja akiibua lake.