Wanawake Zijueni Dalili Za Wanaume Ambao Sio Waoaji

Wahenga wanasema raha ya mapenzi umpate akupendae ingawa watu wengi wamekuwa wakiumizwa na mapenzi na watu wanaojulikana kama Matapeli wa mapenzi.

Wapo ambao wamekata tamaa kabisa, hawataki kusikia kitu kinachoitwa ndoa maana kila walipojaribu kutupa karata wamejikuta wakiambulia maumivu. Hivyo wanaona bora kuishi kivyaovyao tu.

Ni vyema kujua dalili za mwanaume ambaye sio muoaji ambaye yupo kwa ajili ya kukuzuga:

1.Atakutafuta Wakati Wa Kukutana kimwili tu 

Yupo kwako kwa ajili ya maslahi fulani na baada ya muda atakuacha  mtu ambaye yupo kwako halafu hana muda na wewe zaidi ya kukuhitaji tu kwa ajili ya kujiburudisha, huyo anza kumtilia shaka.

2. Mwanaume ambaye sio muoaji atajifanya ni mpenzi wako lakini pia hapendi umjue sana.

Hahitaji uingie kwenye maisha yake kiundani, mnakutana tu barabarani au hotelini biashara imeishia hapo. Hataki kukutambulisha kwa ndugu au hata marafiki. Ukimuona yupo hivyo, anza kuwa naye makini.

3. Hatakuwa na Maongezi ya Maendeleo na wewe.

Wanaume matapeli mara nyingi huwa wanakuwa hawapendi sana kuzungumza mipango endelevu na watu wao. Mwanamke anapoanzisha tu habari hizo, anaruka fasta na kuchomekea mada nyingine. Hayupo tayari, hawezi kukuvumilia uanze kuzungumza habari za sijui kuwa na familia, kuwa na watoto na mambo mengine kama hayo. Anataka mzungumzie zaidi viwanja vya starehe, kula raha na kumaliza mahitaji yake ya kimwili. Baada ya hapo, hana mpango tena na wewe.

4. Atakudanganya kila nafasi atakayopata

Ukimuona mwanaume anakuwa muongomuongo, hana kauli moja katika maisha yenu hiyo pia ni dalili mbaya. Mwanaume ambaye ana nia thabiti ya kuwa na wewe, hawezi kuwa mjanjamjanja. Kama ni sanaa hizo atazifanya kwa watu wengine lakini si kwako.

Mambo Ya Kufanya Ili Kuzuia Marafiki Kuingilia Mapenzi Yenu

Kwenye mapenzi ni vizuri kwa kila mmoja kuwa na marafiki nje ya Mahusiano hii itasaidia kupeana nafasi na kila mtu kupata muda wa kufanya mambo yake bila kufuatana fuatana na kubanana muda wote.

Hata hivyo kuna wakati  marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi.

Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.

1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine 
Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.

2. Upekee wa mambo.
Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.

3. Mwenye maamuzi ni wewe.
Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua.

4. Kuwa na subira.
Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka  unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza kuzitumia kupata suluhu ya tatizo.

5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu: 
Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine.

Mambo 5 Ya Kufanya Ili Mahusiano Yako Yadumu

Mahusiano yoyote yanahitaji kazi, hakuna mahusiano marahisi yanahitaji kutunzwa na wawili mliopo kwenye uhusiano ili yaweze kukua na kumea.

Kiukweli kabisa hakuna binadamu aliyekamilika wote tuna mapungufu yetu kwaiyo ni muhimu kutafuta njia mbali mbali zitakazotuwezesha kukaa kwenye mahusiano pamoja na kuelewana.

Watu wengi tunaingia kwenye mahusiano kwa sababu kuna kitu au vitu vilituvutia kutoka kwa wapenzi wetu lakini hiyo haitoshi inabidi muingie kwenue mahusiano na mtafute njia za kuweza kupendana na kuheshimiana kwa wakati mmoja ili muweze kudumu.

Katika kuhakikisha hilo leo nakuletea mambo 10 muhimu ya kufanya ili mapenzi yako na mpenzi wako yadumu:

1. Mawasiliano kwa ujumla

Kwenye mapenzi maongezi ya mara kwa mara na ya dhati na ni kitu muhimu sana. Ni muhimu kwa wapenzi kukaa chini na kuongea itasaidia kuwaleta pamoja na nyie kufahamiana vizuri na kila mmoja atajua nini kinaendelea kwenye maisha ya mwenzake.

2. Utayari wa kuvumiliana

Ili mapenzi yenu yadumu ni lazima wewe na mpenzi wako mjidhatiti katika kivumiliana hasa mkigombana au mkipitia magumu yoyoye kimaisha huuikimaanisha ili uhusiano wenu udumu ni lazina kila mmoja amvumilie mwenzake sio mmegombana kidogo tu unataka muachane au mmekosa pesa basi unataka ukamtafute mwingine.

3. Kukiri kosa na kuomba radhi

Ili mapenzi yenu yadumu lazima mjue kuna kukosea na ni muhimu pale unapokosea umuombe mpenzi wako msamaha hii itawasidia kiheshimiana zaidi. Wote tunakosea hakuna binadamu mkamilifu hivo ni muhimu kujifunza kutoka kwenye makosa yetu.

4. Kuheshimiana

Hakuna kitu muhimu kwenye mapenzi  kama heshima ni minimum kila mmoja amheshimu mwenzie hii itasaidia kuweka mipaka fulani katika mahusiano na hii itoke pande zote mbili mwanamke amheshimu mwanamke na mwanaume hivyo hivyo.

5. Jengeni Urafiki

ili mapenzi yenu yadumu ni lazima muwe na ukaribu na urafiki ilk muweze kuwa karibu na ili mpenzi wako aweze kukwambia kitu chochote ni lazima mjenge ukaribu ilmuambiane kila kitu lakini hapa pia muwe makini Latina kiwe na mipaka ili msije shindwa kufanya mambo yenu mambo yenu.