“Nina Mpango Wa Kuirudisha TMK Wanaume”- Mh. Temba

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Amani Temba maarufu kama Mh. Temba amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kuirudisha Kundi lao la Wanaume TMK.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mh. Temba amesema Kundi la TMK Wanaume litarudi na kuanza kazi ya muziki kama lilivyokuwa zamani ili Kuthibitisha hilo, Temba alisema anatarajia kuandaa kolabo moja matata mwaka huu wa 2019 ili kurudisha rasmi kundi hilo.

Nitawalea wimbo ambao utakuwa na vichwa vyote vya TMK Wanaume niliousimamia mimi, nataka kukata kiu ya mashabiki waliokuwa wanatamani kutuona pamoja”.

Lakini pia Temba alisema wanatarajia ujio wao huo kuwa wa tofauti kwa kubadilisha mfumo wa utendaji wa kazi kutoka wimbo kuwa na dakika tano na kuwa dakika tatu.

Kundi la TMK Wanaume lililokuwa na wasanii wakongwe kama Chege, Temba, Juma nature na wengineo lilivunjika miaka ya nyuma Baada ya mgogoro mkubwa kuhusu uongozi na maslahi.

“Mh. Temba Alimfumania Mke Wake, Walishaachana” – Bi. Cheka

Msanii wa Bongo fleva aliyetamba miaka ya nyuma na nyimbo zake kama ‘Ni wewe’ ‘Naenda kusema kwa mama’ na nyinginezo nyingi Bi. Cheka aliyehipatia umaarufu baada ya kuwa msanii mzee kuliko wote amerudi upya kwenye headlines.

Bi. Cheka amerudi upya hivi karibuni baada ya kumrushia tuhuma nzito msanii mkongwe Mh. Temba akidai kuwa yeye na mke wake wameachana baada ya kumfumania mke wake na njemba nyingine.

Chanzo cha ugomvi huu kilianza baada ya Bi. Cheka kudai kuwa kutokana na kuwa na umri mkubwa ameumwa mpaka kukaribia kufa lakini amesikitishwa hakuna hata msanii mwenzake aliyeenda kumuona huku akimrushia tuhuma Mh. Temba aliyeshirikiana naye kwenye wimbo wake wa ‘Ni wewe’ na pia Mkubwa Fela aliyekuwa meneja wake.

Baada ya kumrushia tuhuma hizo Mh. Temba aliibuka na kusema kuwa hawezi kufikia maanani sana anachokisema Bi. Cheka kwa sababu ni mzee hivyo sio kosa lake.

Baada ya kusikia jibu hilo Bi. Cheka hakupendezwa alimwaga povu zito Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv ambapo alifunguka haya mazito kuhusu Mh. Temba na mkewe:

Kwanza huyo Mh. Temba mbona hasemi kuwa mke wake kapata bwana mwingine aseme ukweli hapa alimfumania ndani ya nyumba yake mwenyewe akiwa na mwanaume mwingine ya kwake mazito kuliko ya kwangu mbona yake siyaingilii wala sina habari nayo”.

Bi. Cheka aliongea kwa uchungu akidai amekerwa na usaliti aliofanyiwa kwani alitegemea Temba na TMK watamkubuka akiugua kama ilivyokuwa zamani wakati marafiki.

Mh.Temba Asema Sababu Za Kuvunjika Kwa Ya Moto Band

Imekuwa ni kama desturi kwa baadhi ya makundi mengi ya muziki kuvunjika na kushindwa kuendelea kufanya kazi pamoja, ilhali wanakuwa tayari walishateka soko la muziki na mioyo ya mashabiki wa muziki, ndicho kilichotokea kwa kundi la muziki wa Ya Moto Band , kundi lililokuwa likifanya vizuri na kupendwa na watu wengi katika muziki wao waliokuwa wanaufanya,lakini pia umaarufu wao haukuwa tu nchini Tanzania bali hata nje ya nchi, .Kwa sasa kundi ilo la muziki limevunjika huku kila msanii akitafuta ustaarabu wake wa kufanya kazi zake za kimuziki, inaweza kuwa bahati nzuri au kipaji cha msanii ndicho kinaweza kumpelekea kuendelea kufanya vizuri katika muziki kwa upande wao.

Sababu za kuvunjika zimekuwa nyingi lakini hakuna anaekuja na jibu kamili kuhusu kuvunjika kwa kundi ilo , Mh. Temba ameibuka na kuongelea sababu za kuvunjika kwa kundi ilo, akiwa kama mmoja wa waanzilishi na mlezi wa kundi ilo la muziki tangu wakiwa chini mpaka wameanza kujulikana Mh. Temba anaasema kuwa shida kubwa ya kuvunjika kwa kundi ilo ni kuvamiwa na watu wenye ela.

Akiongea na East Africa  katika kipindi cha Planet Bongo, Mh.Temba anakiri kuwa kundi ilo lilianza kuingiliwa kati na watu wenye fedha na kutaka kuwamiliki wasanii bila kuangalia wasanii hao wametoka wapi huko nyuma.”mimi nakupa mfano wa hawa Ya moto band,utaona labda mtu anasimamia msanii fulani,,mbona hakumchukua mwanzoni wakati  hajulikani, kabla hatujamkuza na kuwa superstar” alifunguka Mh.Temba

kwa maoni yake anasema kuwa kama hao wenye pesa walitaka kusaidia wasanii basi wanapaswa kutafuta vipaji vipya mitaani viko vingi na wanaitaji kuinuliwa lakini sio kuja kuingilia kwa wasanii ambao tayari walishakuzwa na wana majina tayari’huyo mtu kama anauwezo  kwanini asingekuwa na vipaji vyake,wewe unaona nuru tayari inangaa ndo  unaenda kuchomoa pale” aliongezea Mh. Temba

undi la Ya Moto Band lilikuwa likiundwa na Aslay, Enock Bella, Maromboso na  Beka Flavour, lakini kwa sasa kundi ilo kila mmoja anafanya kazi kwa kujitengemea huku Aslay akiwa  chini ya menejimenti ya Chambuso . Hata hivyo baaada ya kundi ilo kuvunjika msanii anaeonekana kufanya vizuri kuliko wote  ni Aslay huku wengine wakioneka kushindwa kabisa kutokana na ukimya wao.kundi ili kuvunjika na dalili mbaya ya kupotea kwa vipaji vya muziki.