Mzee Yusuph Afungukia Sakata La Kuvamiwa na Majambazi

Aliyekuwa nyota wa muziki wa taarab nchini Mzee Yusuph amefunguka na kueleza sakata la kuvamiwa na majambazi lililotokea siku chache zilizopita.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Mwananchi leo Jumanne Mzee Yusuf ambaye sasa ni mwalimu wa dini amesema pamoja na majambazi hao kumuumiza mkewe ila naye aliwapa kipigo kidogo.

Akisimulia tukio lilivyokuwa, amesema ilikuwa ni majira ya saa 2:30 usiku Jumatatu wakiwa sebuleni wanaangalia TV, wakasikia kishindo cha watu kikitua ndani ya uzio wakajua wamevamiwa na wahalifu.

Mimi kwa haraka nilipochungulia niliwaona wawili nje nikawafuata kupambana nao kumbe walikuwa zaidi ya saba na wawili walikuwa getini.

Huku nyuma watatu wakaingia ndani na kukutana na mke wangu huku wakimtaka awaonyeshe hela zilipo na kumtisha kwa bunduki, ingawa mke wangu haraka sana alibaini ilikuwa bunduki bandia ndipo alipoanza kupambana nao.

Amesema kwenye mapambano hayo kwa sababu walikuwa wengi walimzidi nguvu na kumpiga mateke ya tumboni yaliyopelekea kusikia kizunguzungu na kuanguka.

Baadhi yao tunawafahamu, wanaishi hapa mtaani na mara nyingi majirani wamekuwa wakiwahisi wana tabia hiyo ya wizi ambapk mbali na hilo kumjeruhi mkewe pia wamemjeruhi mtoto wake“.

Mzee Yusuph ametaja vitu vilivyoibiwa mbali na fedha kuwa ni simu na vifaa vya shule vya watoto.

Mzee Yusuph Aombea Dua Muziki wa Taarabu Uanguke.

Msanii mkongwe wa siku nyingi Mzee Yusuph ambae alistaafu muziki na kujikita katika maswala ya din amefunguka na kusema kuwa hajui kuhusu maendeleo ya muziki huo kwa sasa lakini kama muziki huo unakufa basi kwake hana shida zaidi ya kuuombea dua ufe kabisa ili wasanii wake watafute kitu kingine cha kufanya.
Alhaji Mzee Yusuph amesema kuwa kama taarabu inayumba ataomba dua ianguke na watu watafute vitu vizuri zaidi. “Siijui na siisikilizi yaani sijapata nafasi ya kuusikiliza na sitaki kabisa kujua kunaendeleaje kama kuna yumba ntaomba dua zaidi kuanguke kusiyumbe, watafute vitu vizuri zaidi ya taarabu ,” alisema Mzee Yusuph katika mahojiano yake na Azam Tv.
Nimeacha taarabu wakati bado napenda unaelewa huyo kuacha wakati unapenda na nikamuomba Allah nikamwambia napenda hiki kitu lakini nakiacha, sasa nijaalie nikichukie maana yake nimeacha kitu ambapo bado kinaendelea kufanya maisha.”

Mzee Yusuph- Maisha Ni Magumu Tangu Nimeacha Muziki

Aliyekuwa Mwanamuziki wa nyimbo za taarab nchini Mzee Yusuph amefunguka na kuelezea hali yake ya kiuchumi ilivyo ngumu tangu aache kuimba.

Mzee Yusuph alijizolea umaarufu katika sanaa hiyo baada ya kuonyesha umahiri mkubwa na kuopngoza bendi  yake ya Jahazi Modern Taarab.

Siku za nyuma kidogo Mzee Yusuph alitangaza kuachana rasmi na muziki wa Taarab kwa sababu za kidini na kuamua kuachana na mambo ya kidunia na badala yake kumgeukia Mwenyezi Mungu.

Hivi sasa Mzeee Yusuph anafunguka na kueleza jinsi maisha yanavyomuwia ugumu tangu alipoachana na sanaa hiyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni Mzee Yusuph alifunguka haya:

Tangu niache kufanya Muziki wa kidunia kipato changu kimeshuka sana sasa hivi nafanya biashara ya kuuza matofali ila uzalishaji ni mdogo kutokana na kwamba mtaji ni mdogo ila pia kuna changamoto za hapa na pale sahivi kuna mvua na nini”.

Tangu Mzee Yusuph aachane kufanya Muziki inasemekana kuwa muziki huo umeishia kuzorota na hata kufa kabisa.

Ujumbe wa Diamond kwa Mzee Yusuph kufuatia kifo cha mkewe na mtoto wake

Mzee Yusuph alimpoteza mke wake mdogo Chiku Khamis Tumbo na mwanawe mchanga ambao waliaga dunia usiku wa Jumamosi katika hospitali la Amani Dar es Salaam Tanzania.

Chiku alifariki akijifungua, mtoto wake wa kike pia aliaga dunia wakati huo. Mwenda zake alikimbizwa hospitalini na Mzee Yusuph usiku huo alipoanza kuskia uchungu wa kujifungua.

Mashabiki wa Mzee Yusuph wamekua wakitoa salamu za rambirambi kwenye mitendao za kijamii kufuatia kifo cha bibi yake.

Chiku Khamis Tumbo

Diamond Platnumz pia amemfariji Mzee Yusuph kwa ujumbe aliyoandika kwa Instagram; alimpa roho kwa kumwambia Mola ndo hupanga kila kitu duniani.

“Stay strong bro, Mwenyez Mungu ndio mpanga wa kila jambo… tumshukuru na kuwaombea waendapo wapumzike kwa Amani…Amin, Inshaallah?” Diamond aliandika.