Esma Platnumz Athibitisha Mahusiano Ya Petit Man na Karen

Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ ameanika mahusiano ya mumewe wa zamani Petit Man na msanii wa Bongo fleva Karen Gadner.

Miezi michache iliyopita Esma na aliyekuwa mume wake na mzazi mwenzake Petit Man walitangaza kuachana baada ya miaka michache ya ndoa lakini muda mfupi baadae tetesi za Petit kuwa Kwenye Mahusiano na Karen zilianza kusambaa.

Lakini Kwenye mahojiano na Global Publishers, Esma amefanya kama kuweka wazi Mahusiano hayo ambapo aliulizwa endapo Mtoto wake na Petit anamkumbuka baba yake ambaye kwa sasa hawaishi pamoja ndipo alipojibu:

Anamkumbuka tena sana tu sasa atafanyaje na baba yake ndio kashanogewa na penzi jipya la mtoto wake Gadner jamani mbona mnajifanya hamjui wakati mnajua kila kitu kwani hamjui mbona hata wanaishi pamoja jamani sio siri tena”.

Lakini pia Esma ameweka wazi kuwa hana mpango wa Kuolewa Tena kwa sasa lakini ametaja vigezi anavyovitaka kwa mwanaume ili Awe naye Kwenye Mahusiano:

Napenda mtu mzima ambaye kashamaliza ujana halafu ‘Gentleman’ nitulie naye utoto utoto hapana kwa sasa maana kinyago ukichonge mwen-yewe mwisho wa siku kinakutisha mwenyewe sitaki mimi nimejifunza”.

Hatimaye Aliefunga Ndoa ya Petit Ajulikana

Baada ya kuwa na tetesi za muda mrefu kuwa msanii Karen na Petit man wamekuwa na mahusiano ya kimpenzi na hata kufikia hatua ya kufunga ndoa pamoja na kwamba bibi harusi hakuwa akijulikana , basi picha za siku ya harusi zimeanza kusambaa na kwamba wawili hao wamemua kufanya jambo hilo kutokuwa la siri tena.

Mwanadada karen mtoto wa Gadner G Habash ameamua kufunga ndoa ya kimya kimya na Petit man  miezi michache baada ya mwanaume huyo kuachana na mama wa mtoto wake wa kike Esma Platinumz ambae ni dada yake na Diamond Platinumz.

Karren akiwa na baba yake mzazi.

muonekano wa karen