Esma Afungukia Maisha Baada Ya Kuachwa

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka na kuongelea maisha yake Baada ya kuachwa na aliyekuwa mume Wake Petit Man.

Esma amefunguka na kusema kuachika kwake kwenye ndoa hakujamfanya akate  tamaa ya kuendelea na maisha mengine ya kawaida.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Esma ambaye ni mama wa watoto wawili alisema kuna wanawawake wengine wakiachwa huwa wanakuwa kama wamepatwa na ugonjwa wa kuwafanya washindwe kufanya chochote maishani wakiwaza tu mapenzi, jambo ambalo halipaswi kufanywa na mwanamke anayejitambua.

Ukweli ni kwamba kuachika kwangu hakujanifanya nishindwe kuendelea na maisha yangu ya kujitafutia riziki. Kwanza nilipoachwa ndiyo maisha yakaninyookea“.

Esma alikuwa amefunga ndoa na Petit kwa miaka kadhaa kabla ya kuachana mapema mwaka jana Baada tetesi kusikika kuwa Petit alikuwa amempa mimba mwanamke mwingine.

Nampenda Sana Tanasha – Esma Platnumz

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka na kudai kuwa anamkubali sana wifi yake mpya Tanasha kwa muda mfupi ambao amemjua.

Esma ambaye amekutana rasmi na Tanasha siku chache zilizopita amedai kuwa ameshaanza kumpenda ‘kumoyo’ wifi yake mpya Tanasha Donna kiasi cha kujiuliza kwamba, mwana­dada huyo alikuwa wapi siku zote hizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda Esma alisema amekuwa na ukaribu kwa muda mfupi na wifi yake huyo lakini ametokea kumkubali na sasa ame­kaa kwenye moyo wake tofauti na alivyotarajia mwanzo kwani mtu akiwa mpya kumzoea inahitaji moyo kuridhia.

Huwezi amini Tanasha tayari ameshakaa ndani ya moyo wangu, nampenda sana na kuna muda najiuliza alikuwa wapi muda wote? Kwa nini hakutokea mapema kwenye familia yetu? Hayo mambo ya kuniita Yuda hata siyajali kabisa, wata­jua wenyewe kwani mimi maisha yanasonga”.

Diamond alimtambulisha Tanasha kwa Familia yake aliweka mama yake mzazi Mama Dangote siku chache zilizopita.

 

Esma Akiri Kumkumbuka Hamisa Mobetto

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kudai kuwa amemiss sasa Mzazi mwenzake na Kaka yake Hamisa Mobetto.

Esma ambaye amewahi kuwa na urafiki na Mobetto ameweza wazi kuwa mbali ya kuwa wifi yake Lakini aliwahi kuwa rafiki mzuri sana kwake hivyo anakuwa anamkumbuka sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Esma  alisema kati ya watu ambao huwa akikaa anawamisi, mmojawapo ni Mobeto kwa kuwa alikuwa ni rafiki mzuri kwake ingawa watu wengi hawalijui hilo.

Sijasema hivi kwa kutafuta kiki jamani ila nimeongea ukweli kutoka moyoni. Misa (Mobeto) alikuwa ni rafiki mzuri sana kwangu ingawa siku hizi kuna watu kwenye mitandao wanamuaribu na amekuwa tofauti na mwanzo”.

Urafiki wa Esma na Mobetto ulifikia kikomo mara Baada ya Diamond kumkataa Mtoto wa Mobetto na kusababisha ugomvi kati ya panda hizo mbili.

“Marafiki Wanamuharibu Hamisa”- Esma Platnumz

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ ameibuka na kudai Hamisa ni rafiki mzuri sema watu wanatajwa kama marafiki zake ndio  wamemuharibu.

Esma amefunguka hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo aliomba mashabiki zake wamuulie maswali yoyote na yeye angejibu na moja kati ya maswali aliyoulizwa yalimuhusu Hamisa.

Kama utakumbuka siku za nyuma Esma alishawahi kuwa na urafiki wa karibu na Hamisa Mobetto tena inasemekana alikuwa na urafiki na familia ya Diamond kwa miaka mingi.

Lakini urafiki huo uliingia shubiri baada ya Hamisa kuzaa na Diamond na kupelekea Bifu kubwa kati ya Hamisa na Familia nzima ya Diamond iliyopelekea urafiki wa Esma na Hamisa kuisha kabisa.

Swali la Kwanza:

Umemiss nini kutoka kwa Hamisa Mobetto alikuwa rafiki Yako sana?

Esma Akajibu:

Hamisa ni rafiki mzuri ila watu wanamuharibu tu”.

Swali la Pili:

Kwa nini hupendi Hamisa aolewe na Diamond?

Esma Akajibu:

Sijawahi kusema hivyo”.

Sakata la Hamisa na Esma lilichukua sura mpya Baada ya kumrushia tuhuma za uchawi dhidi ya kaka yake Diamond.

 

Esma Ashabikia Ndoa Ya Diamond na Tanasha

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka  na kuweka wazi mapenzi yake kwa wifi yake mpya Tanasha na kuweka wazi kuwa kama kaka’ke huyo atachukua uamuzi wa kumuoa kwake yeye anabariki kwa sababu ni chaguo lake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Esma hadhani kama ni vyema kumchagulia kaka yake huyo mke, bali macho yake ndiyo yanaona wapi ni bora aangukie hapo na atakapopachagua na kumuonesha atampokea tu.

Unajua hata leo Diamond  akimtambulisha rasmi Tanasha kuwa anataka kumuoa, mimi kama dada, nitaona ni jambo la heri kwenye familia yetu ambayo kila kukicha tunamuombea apate mke bora”.

Diamond alianzisha mapenzi na binti huyo wa Kikenya Wiki chache  zilizopita  Lakini wamekwisha tangaza ndoa yao ambayo itafanyika mwezi wa pili mwakani.

Petit Man Athibitisha Kuwa Hana Bifu na Familia Ya Esma

Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache amefunguka na kuweka wazi kuwa hana Bifu na familia ya aliyekuwa mke wake Esma Platnumz.

Petit amesema kuwa hata Baada ya kuachana na Esma Platnumz amekuwa hana tatizo na familia yake na ndio mama yeye na mkwe wake Mama Diamond bado wanaongea vizuri bila tatizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mtandao wa Dizzim Online, Petit Man amefunguka haya:

Sina ugomvi wowote na familia ile, ndio maana hadi leo unaona mimi na mama tunaongea vizuri tunakomentiana vizuri kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi“.

Petit Man na Esma waliachana miezi michache iliyopita Baada ya kuishi kwenye ndoa kwa miaka minne na kuzaa Mtoto mmoja pamoja.

“Nampenda Sana Wifi Yangu Tanasha”-Esma Platnumz

Dada wa staa wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kusema hana neno na wifi yake mpya Tanasha Donna Oketh.

Wiki iliyopita Diamond alimtambulisha Mpenzi Wake Mpya na mara moja kutangaza kuwa ana mpango wa Kumuoa itakapofika mwakani tarehe 14 February.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi, Esma ambaye alikuwa beneti na Tanasha alifunguka kuwa kwa upande wake alimpokea wifi yake mpya kwa mikono miwili.Esma ambaye amepachikwa jina la Yuda mitandaoni kutokana na kuwageuka warembo ambao huwa wanakuwa na Diamond kisha kupigwa kibuti alisema:

Wala sina shida, nimemkubali wifi yangu na kwa sababu Nasibu (Diamond) mwenyewe ndiye amesema anamuoa na ameridhiana naye, mimi ni nani nikatae?

Kikubwa ninawaombea heri tu asiwe kama wengine ili na mimi nipate wifi wa halali, niache uyuda”.

Mashabiki wameituhumu familia ya Diamond kwa unafiki kwani Wiki mbili tu zilizopita walionekana na Kim Nana na hata Mama Diamond alisema mume Wake anamfundisha dini ili aweze kubadilisha dini na kuolewa na Diamond.

Esma Platnumz Amuweka Wazi Mpenzi Wake Mpya (picha)

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amemuanika mpenzi wake  Mpya kwa Mara kwanza kwenye mitandao ya kijamii tangu Atangaze mahusiano mapya.

Miezi michache iliyopita Esma aliachana rasmi na aliyekuwa mume Wake ndoa Petit Man Wakuache Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka kadhaa.

Esma aliweka wazi kuwa sababu ya kuvunja ndoa yao ni pale alipogundua kuwa baba watoto wake huyo amechepuka na mwanamke mwingine na ameishia kumpa mimba.

Esma ametumia social media kumuanika Mpenzi Wake Mpya ambapo ameweka picha zake na kusindika na maneno matamu ya kimahaba akiwa ameandika:

Roho yangu furaha yangu kipenzi changu umeniambukiza ugonjwa wa mapenzi naona Kama dunia nzima tuko wawili tu”.

Esma Adai Anajenga Nyumba Ili Kukwepa Aibu

Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Esma Khan amefunguka amefunguka an kuweka wazi nia yake ya kujenga nyumba ili kuondoa aibu hapo mbeleni.

Esma Platnumz ameweka wazi kuwa anaogopa kuaibika kama ambavyo hutokea kwa mastaa wengi wanapotangulia mbele za haki na kukosa mahali pa kuagiwa.

Katika mahojiano yake aliyofanya na Global Publishers, Esma amedai amejifunza kwa mastaa wengi ambao walikuwa wanatamba mjini, lakini walipofariki dunia ndipo maisha yao halisi yakagundulika ikiwemo kutokuwa hata na nyumba wakati enzi za uhai huonekana wakiishi maisha ya kifahari.

Naogopa kuaibika ndiyo maana nimenunua kiwanja maeneo ya Madale (Dar), natarajia kuanza kujenga hivi karibuni ili hata nikifa, watu wasipate shida ya mahali hata pa kuagia”.

Esma ameachana na mume wake wa miaka kadhaa Petit Man miezi michache iliyopita na kudai hana haraka ya kutafuta mwanaume mwingine kwani yupo busy na kulea watoto wake.

Esma Platnumz Athibitisha Mahusiano Ya Petit Man na Karen

Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ ameanika mahusiano ya mumewe wa zamani Petit Man na msanii wa Bongo fleva Karen Gadner.

Miezi michache iliyopita Esma na aliyekuwa mume wake na mzazi mwenzake Petit Man walitangaza kuachana baada ya miaka michache ya ndoa lakini muda mfupi baadae tetesi za Petit kuwa Kwenye Mahusiano na Karen zilianza kusambaa.

Lakini Kwenye mahojiano na Global Publishers, Esma amefanya kama kuweka wazi Mahusiano hayo ambapo aliulizwa endapo Mtoto wake na Petit anamkumbuka baba yake ambaye kwa sasa hawaishi pamoja ndipo alipojibu:

Anamkumbuka tena sana tu sasa atafanyaje na baba yake ndio kashanogewa na penzi jipya la mtoto wake Gadner jamani mbona mnajifanya hamjui wakati mnajua kila kitu kwani hamjui mbona hata wanaishi pamoja jamani sio siri tena”.

Lakini pia Esma ameweka wazi kuwa hana mpango wa Kuolewa Tena kwa sasa lakini ametaja vigezi anavyovitaka kwa mwanaume ili Awe naye Kwenye Mahusiano:

Napenda mtu mzima ambaye kashamaliza ujana halafu ‘Gentleman’ nitulie naye utoto utoto hapana kwa sasa maana kinyago ukichonge mwen-yewe mwisho wa siku kinakutisha mwenyewe sitaki mimi nimejifunza”.

Esma Platnumz Amkingia Kifua Wema

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kumkingia kifua Wema Sepetu kutokana na sakata linaloendelea hivi sasa Kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya juzi Wema alimtambulisha mpenzi wake mpya ambaye amedai ndiye atakuwa mume wake mtarajiwa lakini moja kwa moja hali ilibadilika kwani mwanaume yule ameshawahi kumtukana Wema.

Mashabiki mbali mbali wa Wema walimshauri avunje Mahusiano na mwanaume yule na wapo hata Mastaa Wenzake ambao walimshauri atulie kwani mwanaume yule tayari ana wake wawili.

Lakini Esma ameibuka na kumpa sapoti Wema na kulpongeza kwa maamuzi  yake na kumtaka kufanya  kile ambacho moyo wake umeridhia na kama anataka Kuolewa na yule mwanaume basi ruksa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esma ameandika maneno haya kwenda kwa Wema:

Go go Mu forever wiii cha muhimu ukiwa naye uko happy, ifike mahali tuheshimu hisia za watu jamani tutapangiana maisha mpaka lini? Insta imekuwa sehemu ya watu kutuchagulia maisha watu tuishi vipi khaaa Wema ngoja na mimi nikitoe kibabu changu”.

 

Esma Awaita Watoto wa Kaka Yake Kima, Mashabiki Wachukizwa.

Dada wa msanii mkubwa wa bongo fleva nchini,  Esma Pltinumz amefunguka na kuweka picha katika ukurasa wake wa instagram huku akisema kuwa   vikima hivyo kwa sasa vimekuwa na kuviombea kheri na baraka tele.

Jina hilo la kuwaita watoto kima lilianzia pale Diamond alipoamua kuwadharirsha wanawake aliozaa nao watoto na hata kuwaita watoto wake kima  akiamini kuwa kufanya hivyo anaweza kuwaumiza zaidi mama wa watoto hao kumbe pia anawaumiza watoto hao kwa kukuta kumbukumbu ya kitu hicho katika mitandao.

Lakini pia pamoja na kwamba familia hiyo imekuwa ikichukulia neno hilo kama utani, limekuwa likiwachukiza baadhi ya mashabiki na kuona kuwa kinachofanyika cha kuwaita watoto hivyo sio sahihi hasa pale inapokuwa inarudiwa rudiwa na baadhi ya watu wa karibu wa familia ya msanii huyo.

Alichoakindika Esma na kile alichojibiwa na shabiki.

Tabia hii imekuwa kma marudio kwa familia hii na kuchukilia jambo hilo kuwa ni mzaha lakini imekuwa ikiwaumiza baadhi ya watu wanaopita na kuona majina haya.

 

Esma Platnumz-Siwezi Tena Kumshauri Mama Yangu

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan maarufu kama Esma Platnumz amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi Tena kuwa mshauri wa mama yake Bi Sandra maarufu kama Mama Diamond.

Familia ya Diamond inafahamika sana Kwenye mitandao ya kijamii kwa kupendelea kuanika mambo yao Kwenye mitandao ya kijamii lakini sasa Esma amepasua kuwa yeye ndiye alikuwa mshauri mkubwa wa Mama yake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Esma ameweka wazi kuwa kwa sasa amestaafu rasmi kumpa ushauri mama yake kwani nafasi hiyo imezibwa na Baba yake wa kambo.

Nilikuwa ninampa ushauri kama mwanaye maana mimi ndiye mtoto wake mkubwa, lakini kwa sasa mama ana mume wake ambaye ni Anko Shamte kwa hiyo ndiye mshauri wake, sisi tunakaa pembeni”.

 

Mbosso Afungukia Ukaribu Wake na Esma Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Label ya WCB anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Hodari’ Mbosso amefunguka na kuelezea uhusiano wake na Dada wa CEO wa WCB Diamond Platnumz, Esma Platnumz.

Mbosso na Esma wameonekana kuwa na ukaribu sana hasa Kwenye mitandao ya Jamii ambapo wamekuwa waki piga picha mara kwa mara na kuzirusha mtandaoni.

Kwenye mahojiano na waandishi wa Habari, Mbosso amesema Esma ni mshikaji wake sana na huwa wanaimba wote baadhi nyimbo na mara nyingi humfundisha kuimba pia hufikia kipindi hadi anamshawishi na yeye aweze kuimba yaani ajiingize kwenye mambo ya muziki.

Lakini pia mbali na kuongelea ukaribu wake na Esma lakini pia amekanusha vikali taarifa zilizokuwa zinasema kuwa yeye ana mahusiano na dada mwingine wa Diamond ambaye pia ni msanii Queen darlin,na kusema hama mahusiano nae kabisa.

 

Esma Ataja Sifa Za Mwanaume Anayetaka Kuwa Naye Baada Ya Kumwagana Na Petit

Dada wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’amefunguka na kutaja sifa za mwanaume anayetaka kuwa naye sasa baada ya kumwagana na mume wake Petit Man.

Siku ya jana Esma aliweka wazi kuwa yeye na Petit waliachana kipindi kirefu kidogo na kisa cha kuachana kikiwa ni Mumewe kuzidisha kuwa na michepuko.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Esma ameweka wazi kuwa yeye ndio alimuacha Petit na kabla hajamuacha alimfuata mama yake na kumwambia matatizo ya Mumewe na kukiri kuwa mama yake alimsema sana.

Lakini pia amesema hivi sasa anatafuta nyumba ya peke yake ili aweze kuanza maisha mapya peke yake na pia ametajwa sifa za mwanaume ambaye atapenda kuwa naye Kwenye Mahusiano kwa sasa:

Kwanza  mwanaume ambaye namuhitaji ni mwanaume gentleman anayejielewa, mwenye kazi yake nzuri, Awe sio mtu wa drama na Instagram yaani Awe yule mwanaume ambaye yuko straight tunapanga kufanya kitu fulani tunafanya yaani in short nataka mwanaume anayejielewaa kama mimi mwenyewe”.

 

Esma Akana Tuhuma Za Kula Njama Za Kumchafua Mobetto

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kuandika waraka mrefu wa kukana tuhuma zinazomkabili yeye na kama yake za kumchafua Hamisa Mobetto.

Siku mbili hizi kuna taarifa zilienea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Hamisa Mobetto ameenda kwa mganga wa kienyeji kwa nia ya kuwatengeenezea dawa Familia ya Diamond impende na yeye aolewe na Diamond.

Lakini kuna taarifa nyingine ziliibuka kuwa voice note ambaye Esma na Mama Diamond walisema ilikuwa ni Hamisa Akiongea na mganga ilikuwa ya uongo na inasemekana voice note hiyo ilikuwa imepikwa na Mama Diamond kwa nia ya kumchafua na kumpoteza Mobetto.

Baada ya Tuhuma hizo Esma ameibuka na kudai kwamba yeye pamoja na mama yake hawawezi fanya kitu kama hicho kwa Mobetto.

Dada bora ukae kimya halafu unapata zambi kumshilikisha Mwenyezi Mungu ktk swala km hili kuongopa vitu mbona sie wenyewe tupo Kimya au ndio mnatapatapa embu mjitulize jamani hata MUNGU HAPENDI kwani ye ndio Muamuzi plz naomba msinitungie uongo wa kijinga jinga mlichokifanya wenyewe mnakijua na nafsi zinawasuta sipendi kuniingiza ktk uongo wa kijinga msijisafishe kutaka kuchafua watu. Huyo huyo mama mnaotaka awapende kutwa mnachamba na kumtungia uongo naombeni mkitaka kuweka uongo wenu bora mniweke mimi sio mamaangu. MLICHOFANYA MNAKIJUA
#temporarypost?#mfaMajiHamuishiKutapatapa”.

Lakini pia Esma aliongeza:

Katika maisha ni vema kukaa kimya pindi ukikosea na hasa ukijua wazi kuwa nimekosea ila ukijaribu kufuta au kusawazisha kosa kupitia njia za wasiogusa maisha yako ujue kosa linazaa kosa…Ungetulia maana watu wameshiba vielelezo na ushahidi 100%”.