Ukiona Dalili Hizi Ujue Mpenzi Wako Anachepuka

Mapenzi ni matamu lakini huingia shubiri pale mambo yanavyoenda mrama. Je umekaa kwenye uhusiano na mumeo/mkeo/ mpenzi wako kwa muda mrefu kwa raha na amani lakini ghafla unaanza kuona mambo yanabadilika?

Wanawake wengi na wanaume wengi hawataki kuamini yule umpendaye anaweza akachepuka lakini ndio hivyo wengi wao huishia kuwa wasaliti kwa wapeenzi wao.

download latest music    

Hizi ni dalili atakazo zionyesha mpenzi wako akiwa anachepuka:

1. Matumizi Makubwa Ya Mtandao wa kijamii 

Kwa ulimwengu huu wa sayansi na teknologia na uwepo wa utandawazi simu za mkononi zinatumika sana kuficha maovu yaani ukishaona mpenzi wako anaweka na kubadilisha password kila siku, anatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii na kupendelea kuweka picha akkiwa peke yake na kusema kuwa hana mke au mume basi mchunguze vizuri mpenzi wako maana huwezi jua.

2. Atabali Muonekano wake au Mavazi

Ukikaa na mpenzi wako kwenye mahusiano kwa muda mrefu na umeshamzoea kwa kufanya vitu fulani au kuvaa mavazi fulani lakini ghafla unashangaa anabadilika anavaa tofauti anatumia muda mwingi kujibadilisha kama umri umeenda utaona anaanza kubadilisha mavazi ilimradi tu awe tofauti basi hutakuwa na jingine la kufanya zaidi ya kumuangalia mpenzi wako kwa karibu maana dalili zote zinaonyesha inawezekana anachepuka.

3. Mlalamishi/ Mrusha Lawama 

Mtu yoyote anayefanya kosa basi ana kawaida ya kujishtukia hii inatokana na yeye kujisikia vibaya kwa vitendo anavyokufanyia kwaiyo ukiona mpenzi wako anaanza kukusingizia vitu kama vile kwa nini una ukaribu na marafiki zako wa jinsia tofauti na wewe basi jua wazi kabisa anafanya hivyo kwa sababu hivyo ndio vitu yeye anafanya.

4. Mawasiliano Yatapungua

Mkiwa kwenye mahusiano hakuna kitu cha muhimu kama mawasiliano kwani ndio kitu ambacho kitawafanya muwe karibu kwaiyo ukishaona mpenzi wako haongei na wewe mkikaa hamna cha kuongea au saa nyingine anaona hata mzigo kukaa chini na kuongea na wewe basi jua wazi kuwa mpenzi wako huyo anachepuka.

5.  Kutumia Simu Kwa Siri

Simu za mkononi zinachukua nafasi kubwa katika kuharibu mahusiano ya watu ghafla utaona mkiwa pamoja simu yake anaweka mbali au hata ikiita mbele yako hawezi kupokea akaongea kwa uhuru hivyo ataenda kuongelea nje au hata chooni au hata akipokea mbele yako hatakuwa na uhuru. Mkiwa mbali ukipiga simu yake basi itakuwa inatumika mara kwa mara.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.