Rayuu Agomea Ndoa, Asema Kuolewa ni Utumwa.

Wakati watu wengine hasa wasichana katika tasnia wakililia ndoa na kutamani kuingia katika taasisi hiyo, msanii wa maigizo  nchini mwanadada  Alice Bagenzi maarufu kama Rayuu anasema kuwa kuolewa ni swala la utumwa na ufungwa  kwaiyo mtu anapotaka kuolewa ni lazima awe makini sana kuingia uko kabla hajajutia uamuzi wake.

Rayuu anasema kuwa swala la kuoa au kuolewa linahitaji umakini sana  na katika mahusiano mpaka kuamua kufunga ndoa ni lazima watu hao wawe wameamua kweli kuingia katika ndoa hiyo bila kuwa na shinikizo la aina yoyote ile.

download latest music    

Rayuu anasema kwake yeye changamoto kubwa ya ndoa huwa anawafikiria sana mawifi na mama mkwe kwa sababu hao wanaweza kukufanya ukaacha hata ndoa.

kuolewa au kuona ni ufungwa kwakweli na kama kuna muda kila mtu ni lazima akae anamlinda mfungwa wake,ukichemka tu lolote linaweza kutokea na ndoa ikaota mbawa ikapepea na kila mtu akabaki analia tu au kujutia bila kujua ufumbuzi wa tatizo lenyewe.

Rayuu anasema kuwa hata kama watu wanapendana kiasi gani inafika sehemu ni lazima kila mtu amlinde mwenzi wake hasa kutokana na maneno mengi yanayokuwa yanaletwa na ndugu, Rayuu anathibitisha kuwa ndugu wanaweza kuwatenganisha kwa kiasi kikubwa sana hata kama mna kuwa na mapenzi ya kupitiliza.

Rayuu pia ni moja ya wasanii wa bongo movies ambao wanaosemekana kuachika katika ndoa zaidi ya mara moja.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.