Chemical Amshauri Alikiba Siku ya Ndoa Yake.
Mwanamuziki rapper wa kike bongo Chemical amefunguka na kumshauri Alikiba kama aliweza kuweka mahusiano yake kuwa siri basi na maisha yake ya ndoa inabidi yawe hivyo hivyo ili kulinda heshima ya ndao hiyo.
Akiongea na Clouds Tv leo alisema”namshauri aendelee kuweka mahusiano yake kuwa ya siri hivyo hivyo kama ambavyo alifanya katika mahusiano, kwa sababu maisha ya ndoa ukishayaweka wazi baadae yanakuja kukuumiza.kama hivyo alivyoamua kuweka private basi aendelee hivyo hivyo ilimradi tu wenyewe wawe wanaelewana , ampende mke wake maana yeye ni star.
Alikiba amefunga ndoa leo huko mombasa na mpenzi wake wa siku nyingi Amina Rikesh, ndoa ambayo imekuwa gumzo sana katika mitandao ya kijamii.