Barnaba Akana Kuwa na Mpenzi kwa Sasa.
Mwanamuzki barnabas amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mpenzi kama imekuwa ikizushwa katika mitandao ya kjamii na kwamba kama atapata mpenzi hivi karibuni atakuja kumtambulishwa kwa mashabiki zake siku atakapofunga naendoa au kumvalisha pete na wala sio vinginevyo.
Barnaba ameyasema hayo ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu kusambaa kwa baaadhi ya picha katika mtandao wa kijamii zikimuonyesha akiwa na moja ya warembo studio na maeneo tofauti ya kujivinjari huku mazingira yakiwaonyesha kama wapenzi lakini amekataa na kusema hana mahusiano na wanamke yoypote kwa sasa.
sijui chgochote kwa sasa,nilisema siku nitakayo muonyesha mwanamke wangu ni siku namuoa au namvalisha pete tu na sio vinginevyo , siwezi kuwa na mapenzi ya mtandao na mwanamke wangu na kwa mtu nimpendae siwezi kumuweka katika mtandoa hata siku moja,