Hakuna Ninaemwamini Tangu Ninyweshe Madawa ya Kulevya:-Esther kiama
Mwanadada anaefanya vizuri katika anga za bongo movies Ester Kiama amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake amejifunza kutokumuamini mtu yoyote kwa sababu hata waliompa dawa za kulevya hakuwahi kuwadhania kama wataweza kumfanyia hivyo.
Ester anasema kuwa maruweruwe ya kuweka madawa ya kulevya bado hayajamuisha na kwamba pamoja na kwamba alikwenda hospitali na kutibiwa lakini amekuwa muoga mpaka vitu vingine ninaogopa kununua dukani.Ester anasema kuwa amekuwa akiogopa sana vitu vya maji maji kwa sasa.
Huwezi amini kabisa nimekuwa muoga hata kutoka nyumbani kwangu kwa sababu hiyo,nimekuwa muoga kupitiliza kabisa sijui huu ugonjwa utaishaje , naona nimepata ugonjwa wa kuwa na wasiwasi.