Naheshimu Ndoa Kama Ninavyoheshimu Dini Yangu.;-Dully Sykes
Mwanamuzii Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mpango wa kufunga ndoa kwa sababu hataki kukurupuka kama wat wengine kwa sababu kitendo cha kuoa ni kuongeza mtu na kama inatokea mnagombana mkashindwa kuelewana ni kuongeza mawazo.
kwa upande wangu mimi ninaheshimu ndoa kama ninavyoheshimu dini yangu,siwezi tu nikaoa na kukurupuka kumuweka ndani mwanamke alafu baadae tunagombana , unakuwa tayari ulishamuweka moyoni unajikuta unaongeza stress tu.
Hata hivyo alipokuwa akiongea na Shadee wa Clouds e aliulizwa kuhusu swala la umri wake kuwa unaenda na miaka hairudi nyuma hivyo anavyochelewa kuoa inakuwaje, Dully alisema kuwa kwake swala la umri sio shida kama watoto tayari anao.
najua umri una kwenda lakini tayari nina watoto kwa sababu unaweza kuwa na ndoa lakini huna watoto na pia nina shukuru sana kwa sababu watoto wangu pamoja na kwamba wote sikai nao lakini ninawapa malezi bora na kitu kikubwa nashukuru Mungu nimelelewa katika maadili ya dini sana ya kiislamu kutoka kariakoo mpaka ninapokaa sasa , nina ishi maisha tulivu kulivyo vile watu wanavyodhani.