Alichoandika Dogo Janja Kwenye Picha ya Uwoya Iliyoleta Utata Mtandaoni
Baada ya picha za Uwoya kusambaa katika mitandao ya kijamii na kusababisha watu kuongea sana juu ya picha hizo huku wengine wakisema kuwa mwanadada huyo na mke wa mtu na mwezi wa Ramadhani umeisha hivi karibuni hivyo hakupaswa kuweka picha hizo katika mitandao ya kijamii mume wake na msanii huyo hajaonyesha ku-mind chochote kuhusu swala hilo zaidi ya kuendelea kumpa kichwa ju ya picha hizo.
Katika picha hiyo aliyoweka irene katika ukurasa wake wa instagram na kulalamika kwanini watu wamekuwa wakimsema kila anapoweka picha katika ukurasa wake Dogo Janja nae alionngezea upande wa maoni na kusema ‘usicheze karibu hii midoli kwa sababu hii midoli hawang’ti”
Picha hizo za uwoya alizopiga akiwa ufukweni zilisambaa katika mitandao ya kijamii huku baaadhi ya wasanii wenzake kama mwijaku akisema kuwa swala hili linamfanya irene kupoteza kabisa heshima yake.