Ngoma ya Champion Nimepewa na Chid Benz ;-Shiloleh
Mwanadada Shiloleh amefunguka na kusema kuwa wimbo wake mpya wa champion ulikuwa ni kama zawadi kutoka kwa Chid benz kwa sababu alimpigia simu na kumwambia kuwa amemtayarishia wimbo na alipomtumia aliupenda na kuingiza vocal zake ambazo sehemu nyingine anaimba akiwa anachana.
Shiloeh anasem hayo alipokuwa akitambulisha wimbo huo wa champion alipokuwa clouds media , na kusema kuwa katika wimbo huo amekuwa togfauti kwa sababu anachana.
ngoma yangu ya champion humo ndani nimechana na ngoma hii nimeandikiwa na kaka yangu Chid benzi, nakumbuka alinipigia simu usiki na kuniambia kuwa kuna zawadi anataka kunipa na kweli alinitumia na mimi nikaingia coko na hata alivyokuja alishangaa.
Shiloleh aliwahi kufunguka na kuwaomba mashabiki kuacha kumsema na kumchukulia vibaya Chid benz kwa sababu kwa sas ameazna kubadilika na hayupo kama vile alivyokuwa zamani zaidi sana anachohitaji ni maombi ili aendelee kuwa sawa.