Wema Sio Mtoto ila Hajielewi:-Mh Shonza
Naibu waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo,Juliana Shonza amepinga kauli ya Wema Sepetu kusema aliyokuwa akiyafanya ni utoto baada ya kuvuja kwa video zake za faragha.Watu wengi wamekuwa wakimuonea huruma mwanadada huyu na kusema kuwa inawezekana kuwa bado anahitaji msaada na msamaha kujifunza
Akiwa mbele ya mwandishi Waziri Shonza amesema “Wema hana utoto wowote bali nikushindwa kujielewa na hivyo baada ya baraza la sanaa adhabu nyingine bado kutoka TCRA”
Aidha Waziri Shonza amesema kama Wizara nayo itamchukulia adhabu na kuwataka wadada wenye tabia za kukaa utupu mitandaoni kuacha tabia hizo mara moja.
hata hivyo tangu kutokea kwa tukio hilo, wema amekuwa akipokea adhabu tofauti kutoka katika mashirikisho mbalimbali ya filamu huku TCRA wakimfungulia kesi .