Idris Aandika Barua ya Wazi kwa Mh Rais Baada ya Kufutwa kwa Sherehe za Uhuru
Mchekeshaji maarufu nchii ambae pia ni moja ya wahamasishaji wakubwa bongo Idris Sultani ameamua kumuandikia mh Rais barua ya kile anachokiamini baada ya kufutwa kwa sherere za kuhadhimisha kupatikana kwa uhuru wa Tanzania.
Idris anasema kuwa kufutwa kwa sherehe hizo kutaathiri sana hali ya uzalendo hasa kwa vijana na watoto waliopo ambao bado wanahitaji kujua historia ya Tanzania.
Idris anasema kuwa anaogopa sana swala la kufutwa kwa sherehe hizo kwa sababu kuna fanya kuptea kwa uazlendo kidogo kidogo ukizingatia kuwa vijana hao ndio watakaokuja kufanya kazi katika ofisi za serikali bila kuwa na historia ya kile wanachokifanyia kazi.
Idris anasema kuwa pamoja na kwamba wanasema pesa za sherehe ziende kwenye matumizi muhimu kama afya lakini ni vigumu kulinganisha vitu hivyo vyote zaidi ya kuwa vinahitajika vyote na ndio maana ni ngumu hata kuchagua kati ya kula na kupumua.