Sugu Avunja Ukimya Juu ya Swala la Malezi ya Mtoto

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Mbunge wa Mbeya mjini amevunja ukimya na kufunguka kwa mara ya kwanza juu ya shutuma zinazomkabili  dhidi ya mzazi mwenzie Faiza Ally.

Faiza amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kumshutumu Sugu kwa kukataa kumlea binti yao mdogo Sasha. Baada ya juzi kumsema Sugu kuwa hamjali mtoto wake na kukataa kumlipia mtoto huyo ada ya shule hadi kufikia hatua ya Sasha kurudishwa nyumbani.

download latest music    

Kwa mara ya kwanza Sugu kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka na kusema anamlipia ada binti yake huyo lakini mwenye matatizo ni mama yake kwani humkataza kumuona, aliandika yafuatayo juu ya tuhuma hizo:

“Huwa sipendi kuposti hivi vitu lakini imenibidi,  hizi ni bank slips za ada ya mwisho niliyolipa kwaajili ya Sasha na ilikuwa mwezi huu wa tisa nimuanzishe shule ya Feza Nursery pale Mikocheni, lakini from no where mama yake ghafla akanizuia na kusema hahitaji nilipe ada na kunizuia nimsomeshe tena Sasha! Na kwamba ana uwezo wa kumsomesha mwenyewe shule yoyote anayotaka na ndo kumpeleka huko Hazina international ambako pia hata hivyo nilishaanza kuwasiliana na uongozi ili niendelee tu kulipa ada hata kama nimepigwa marufuku kumuona mwanangu bila sababu. Hivi kama nyie mngefanyaje?

Hata hivyo mara baada ya kusema hayo Faiza alikuja juu na kumuita Sugu muongo na amewahi kulipa ada mara mbili tu tangu mtoto wao aanze kusoma na miaka yote hiyo Faiza ndo alikuwa analipa ada.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.