Abdu Kiba adai hajamuona wa kushindana na Ali Kiba

Msanii wa bongo Abdu Kiba amefunguka kudai kuwa kaka yake, Ali Kiba, ni msanii ambaye bado hajapata mtu ambaye anaweza kumfikia ikifikia wakati wa kutunga na kuachia nyimbo.

Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds Fm hivi karibuni Abdu Kiba alisema kuwa yeye na Ndungu yake hawapendi kuhusishwa na team za kimuziki au kuonekana wanajipanga kushindana na watu fulani.

download latest music    

Aliendelea kwa kusema kuwa yeye na Kaka yake bado wanafanya kazi ambazo bado hawajapata watu wa kushindana nao.

“Sisi tunachukulia ni changamoto kwa sababu sisi hatushindani, tunafanya kazi na hatujaona bado wa kushindana nao, hakuna mtu wa kushindana na sisi, yaani sijamuona wa kushindana naye na hakuna wa kushindana na sisi na sisi hatushindani,”

 

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua