Abdu Kiba afunguka kwanini hamfollow mtu yeyote ata kaka yake Ali Kiba kwenye Instagram

Kakake Ali Kiba amechukua mkondo kama wa rapa wa kimataifa – Eminem ambaya hamfollow mtu yoyote kwenye mtandao wa instagram.

Eminem ambaye ni mfalme wa rap ako na wafwasi milioni 12.7 kwenye Instagram lakini hamfwati (follow) mtu yeyote kwa Instagram.

download latest music    

Abdu Kiba amechukua mkondo huo pia, msanii huyo wa Bongo Fleva ako na wafwasi laki 384 kwa Instagram lakini hamfwati mtu yoyote hata kaka Ali Kiba.

Abdu alifunguka na kusema kuwa yeye hamfollow yeyote kwasababu hackers waliiba account yake na na alipoirejesha ilimbidi kuwaondoa watu wote waliokuwepo.

“Nikizungumzia akauti nakumbuka mwezi mmoja nyuma nikiwa Marekani akaunti yangu walihack kwa hiyo nilikaa karibia wiki tatu siko kwenye mtandao wa instagram, nilipoweza kuirudisha akauti yangu ndipo nilipoamua nisimfollow mtu yeyote kwa sababu watu niliowakuta mule sio watu wangu. Kwa hiyo niliwa-unfollow nikabakia siwezi kumfollow mtu tena. Sijafuta utaratibu wake bali ni maamuzi yangu, wategemee any day naweza nikamfollow mtu yeyote,” Abdu Kiba alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere