Abdu Kiba akana tetesi za kumuiga Ali Kiba

Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa Alikiba hivi karibuni alifunguka kuelezea kilichotokea baada ya mtandao wake wa Instagram kuibiwa na mtu asiyejulikana.

Msanii huyu ambae amekawia bila kuachia nyimbo mpya alisema kuwa baada ya kurudisha Instagram yake alipata kuwa amewafollow watu ambao yeye hawajui na jambo hili likamfanya kuunfollow kila mtu kama anavyofanya Alikiba.

download latest music    

Alisema haya kukana tetesi zinazodai kuwa anamuiga ndugu yake mkubwa. Alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Nikizungumzia akauti nakumbuka mwezi mmoja nyuma nikiwa Marekani akaunti yangu walihack kwa hiyo nilikaa karibia wiki tatu siko kwenye mtandao wa instagram, nilipoweza kuirudisha akauti yangu ndipo nilipoamua nisimfollow mtu yeyote kwa sababu watu niliowakuta mule sio watu wangu.”

Aliendelea kwa kusema,

“Kwa hiyo niliwa-unfollow nikabakia siwezi kumfollow mtu tena. Sijafuta utaratibu wake bali ni maamuzi yangu, wategemee any day naweza nikamfollow mtu yeyote,”

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua