Abdu Kiba Amefunguka Baada ya Video Yake na Fahyma wa Rayvanny Kusambaa Mtandaoni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye pia ni maarufu sana kwa sababu ya undugu alionao na staa wa Bongo fleva Ali Kiba, amefunguka na kuongea kwa mara ya kwanza kuhusiana na video iliyomuonyesha yeye na mke wa Rayvanny.

Kipindi cha nyuma kidogo kuna video ambayo ilisambaa mtandaoni ambayo ilimuonyesha Abdu Kiba na baby mama wa Rayvanny anayejulikana kama Fahyma au Fahyvanny wakiwa wamepozi wanapiga stori.

download latest music    

Inajulikana wazi kuwa Rayvanny yupo WCB na Diamond ni bossi wake lakini pia inajulikana kuwa Ali Kiba na Diamond ni paka na panya hivyo hiyo inapelekea makundi haya mawili kuwa na bifu hivyo ilipotokea Rayvanny na Fahyma wameachana kisha video yake na Abdu Kiba ikasambaa mtandaoni maneno mengi yalisemwa kutokana na ushindani wa kimuziki uliopo baina ya Ali Kiba na Abdu Kiba dhidi ya timu nzima ya WCB.

Baada ya sakata hilo Abdu Kiba Amefunguka Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo Tv ambapo amedai kuwa anamjua fahyma tangu zamani sana na ile video ni ya kitambo kipindi hicho  fahyma alikuwa shabiki wake.

Nilimjulia yule msichana alikokuwa anafanya kazi kule Tv One na tulikuwepo tunafanya Interview ya television na kati kati ya Interview tukarekodi ile video na kipindi kile alikuwa ni shabiki wangu mkubwa lakini hiyo ilikuwa zamani kabla hajawa na Rayvanny nahisi lakini tangu amekuwa kwenye Mahusiano naye sijawasiliana naye”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.