Abdu Kiba na Timbulo Ndani ya Bifu Nzito Baada ya Kuibiana Nyimbo

Msanii wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba amejikuta kwenye mvurugano na msanii mwenzake Timbulo baada ya kituhumiana kuibina mashairi ya nyimbo.

Wasanii hawa wawili waliingia katika mgogoro mkubwa sana Timbulo na Abdu Kiba baada ya wote wawili kujikuta wanaimba mashairi yanayo fanana huku Timbulo akimtupia lawama na kumuuliza kwa nini atumie mashairi yake.

download latest music    

Kizaazaa hiki kilianza baada ya habari kusambaa kuwa kuna rekodi ambayo imefanywa na Timbulo na kumshirikisha msanii mwingine anayeitwa Promise ambayo inafanana kabisa mashairi na nyimbo mpya ya Abdu Kiba inayoitwa jeraha.

Baada ya hapo kilichotokea ni kila mtu anamrushia mwenzake maneno na kumlaumu kwa kumuibia mashairi. Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Timbulo amefunguka na kusema anamlaumu Abdu Kiba kwa kumuibia mashairi yake:

Mengi yatasemwa lakini ukweli utabaki pale pale mimi ninavyozungumza najua ukweli na Abdu na yule mtu anayehusika kwenye huu wimbo anaujua ukweli anajua stori yake ilivyo alafu kitu ambacho kimenikera tangia mwanzoni ni pale nilipoona wimbo umetolewa halafu wamekosea wamesema wimbo unaitwa promise wakati mwenye wimbo anaitwa promise na jina la wimbo hata silikumbuki lakini mimi namlaumu Abdu maana like alichokiimba Abdu mimi ndio nimetunga mashairi yote aliyoimba”.

Baada ya kutupiwa lawama hizo AbduKiba alifunguka na kusema nyimbo ile kapewa na Promise ambaye ni mmiliki wa nyimbo hiyo na yale mashairi yote yaliandikwa na yeye mwenyewe lakini baadae Timbulo ndio aliomba kuimba mashairi hayo. Abdu Kiba alitoa povu zito huku akidai kuwa Timbulo amemdhalilisha kwa kumnyooshea kidole na kumtuhumu kwa wizi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.