Abdu Kiba- Sitegemei Skendo Kusukuma Muziki Wangu

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa staa wa Bongo fleva Ali kiba amefunguka na kudai hakuna kitu hapendi kwenye maisha yake ya muziki kama skendo.

Wasanii wengi wa Bongo fleva wanategemea skendo au wenyewe wanaita kiki ili kusukuma Muziki wao kwani wakifanya matukio wakakaa Kwenye midomo ya watu basi itasaidia kuwapa airtime ya bure.

download latest music    

Abdu Kiba amesema tofauti na wasanii wengine Muziki wake hautegemei kusukumwa na skendo za mitandao ya kijamii bali ni kazi yake na juhudi zake ndio zinamuweka juu.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Mtanzania, Abdu Kiba amesema wasanii wengi wanaopenda skendo hawajiamini na wao ndio chanzo cha kushusha thamani ya muziki nchini.

Muziki ni maisha yangu na kazi inayonipa fedha za kujikimu mimi na familia yangu, napenda kutoa kazi zenye viwango ndio maana mashabiki wananipenda na kuendelea kufuatilia kazi zangu”.

Lakini pia Abdu Kiba ameweka wazi jinsi skendo zinavowabeba wasanii wengi.

Katika vitu nisivyovipenda kwenye maisha ya muziki ni kuishi kwa skendo, mambo kama haya huwa ni sababu ya kushusha thamani ya mtu na kazi yake”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.