Afande Sele Amkingia Kifua Diamond Baada ya Kufungiwa na BASATA.

Msanii Afande Sele amefunguka na kuongelea swala la msanii Diamond Platinumz kufungiwa kufanya show ndani na nje ya nchi kutokana na kosa lake la kuimba wimbo ambao uliwahi kukatazwa na BASATA Tangu hapo awali.

Mwanamuziki huyo ambae kila siku amekuwa aijonyesha kuwa yeye ni team-diamond anasema kuwa kufanya hivyo kwa BASATA ni adhabu kubwa sana kwa wasanii hao walitakiwa kupewa adhabu ya kujifunza na wala sio ya kuwakomoa kabisa.

download latest music    

Katika ukurasa wake , afande sele aliandika ” Haijawahi kutokea….unacheza faulo kwenye ligi ya ndani lkn unapewa adhabu ya kutoshiriki hadi mechi za kimataifa…Basata ni mfano wa mtu aliyesifiwa kwa mbio hadi amepitiliza kwao…lkn wao kama wazazi wametimiza wajibu kwani bakora moja haimuui mtoto bali humnyoosha ktk njia sahihi ingawa ktk hili la sasa Baraza limetumia panga au rungu kumuadhibu mtoto kitu ambacho kiasi fulani kinaleta ukakasi hata kama mtoto ameonyesha ujeuri kiasi gani…ila ukweli utabakia palepale kwamba Basata ni Jiwe na wasanii ni Nazi hivyo busara ni wasanii nao kutimiza wajibu wao kwa kuomba Radhi…huo ndio uungwana…Sabalkheriiiii…”

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.