Agnes Masogange Aulaani Mwaka 2017

Mrembo na video vixen anayetikisa hapa bongo kwa umbo lake matata Agnes Gerlad aliye maarufu kama Agnes Masogange amefunguka na kuulani mwaka huu wa 2017 kwa mambo yote yaliyomkuta.

Agnes  amefunguka na kudai kiwa anauchukia sana mwaka 2017 kutokana na mambo magumu yaliyompata  akiri kuusubiri kwa hamu mwaka 2018. Agnes Masogange ambaye amjipatia umaarufu baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Belle 9 ‘masogange’ miaka michache iliyopita amekiri kuwa mwaka huu ulikuwa mgumu sana kwake hadi kupelekea kuuchukia.

download latest music    

Mapema mwaka huu Agnes akiungana na wasanii wenzake mbali mbali kama Wema Sepetu, Rommy Jones, Petit Man Wakuache walikamatwa  na kifikishwa kituo cha polisi baada ya kituhumiwa kwa kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya.

Ingawa baada ya tuhuma hizo na kukaa rumande kwa siku chache na uchunguzi kufanyika wengi wao waliachiwa huru lakini Masogange alikuwa mmoja wa watuhumiwa waliofunguliwa mashtaka mahakamani na hivyo kupelekea Agnes kuwa  na kipindi kigumu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Agnes Masogange amekiri kuwa tuhuma hizo zimemfanya mambo yake yamesimama pia amedai biashara zake nyingi zimesimama kwa mwaka huu kutokana na kukosa muda wa kwenda kufatilia kutokana na kuhitajika mahakamani mara kwa mara.

Bora mwaka 2017 uishe na mambo mengine yaendelee  ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwangu kwa kila kitu hasa kwa sababu ya kesi inayonikabili ya matumizi ya madawa ya kulevya labda mwaka mpya ukianza na mambo mengine yataenda vizuri”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.