Agnes Masogange Awapa Kichambo Marafiki Zake Wanafki

Muuza nyago kwenye video au kwa lugha kimjini video queen maarufu Agnes Masogange aliyepata jina baada ya kutokea kwenye video ya msanii Belle 9 inayoitwa Masogange miaka michache nyuma lakini pia amepata umaarufu kutokana na umbo lake la kuvutia.

Kwa miaka kadhaa sasa mrembo huyu amekuwa akiandamwa na kashfa na hata kesi za kujihusisha kwa njia moja ama nyingine na uuzaji au matumizi ya madawa ya kulevya. Kama utakumbuka kipindi cha nyuma alipokuwa anaishi nchini South Africa alishakamatwa na madawa ya kulevya lakini aliachiwa hapo baadae.

download latest music    

Lakini hakuishia hapo kwani mwaka jana alijikuta tena kwenye mkumbo huo huo pale ambapo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alipopitisha msako wake wa wasanii wanaoutumia kuuza au kubeba madawa ya kulevya ambapo baada ya kukamatwa alifunguliwa kesi yake mahakamani.

Tangu kesi yake ianze kusikilizwa mwaka jana mara kwa mara Agnes amekuwa akiuambia umma ni jinsi gani alivyopoteza watu aliodhani ni marafiki zake ambao walimkimbia badala ya kumpa sapoti. Siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Masogange aliwatolea povu zito wale wote alidai wanamfanyia unafki ambapo aliandika:

Pata tatizo ujue rafiki wa ukweli ujue ndugu wa ukweli uwajue hawa tunaowaita dada zetu wa mjini yaani tena watajifanya wako busy na mambo yao lakini ni wepesi kusahau utasikia wanakwambia pliz saidia kushare pliz i beg! yaani usumbufu sitaki mnajijua wanafki wakubwa nyie msione nacheka na nyie nawachora tu”.

Haikujulikana moja kwa moja maneno hayo alimlenga mtu gani lakini Agnes alikiri tangu apate kesi yake ya madawa ya kulevya ambayo bado inaendelea kisikilizwa watu wengi aliodhani ni marafiki zake walimtenga.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.