Agness Alinifanya Nikutane na Dogo Janja:-Irene Uwoya

Mwanadada Irene Uwoya wikiendi iliyopita alifunguka na kusema kuwa kama isingekuwa rafiki yake Agness Masogange ambae kwa sasa ni marehemu basi asingeweza kukutana na Dogo Janja ambae kwa sasa hivi ndio mume wake wa ndoa.

Akiongea na Clouds e , katika sherehe ya ufunguzi wa sehemu ya kuoshea magari iliyofunguliwa na Perfect Chrispin , irene uwoya alisema kuwa mume aliekuwa nae sasa ni agness ndio aliemuunganisha nae na mara nyingi alikuwa akimuongelea sana na ndipo hata yeye aliapoanza kuwa karibu na Dogo Janja.

download latest music    

Irene uwoya na marehemu agness masogange walikuwa marafiki sana  kwa muda mrefu na hata msiba wa mwanadada agness irene alionekana kuumizwa sana na kutokwa na rafiki yake huyo na kuamua kuchora tatoo katika mwili  wake kama kumbukumbu ya kumuweka rafii yake huyo moyoni.

Irene na Dogo Janja walifunga ndoa mwaka jana mwezi wa na ndoa ambayo ilizua mgongano mkubwa sana wa mawazo baina ya watu lakini wao tayari walikuwa wameshaamua kufanya hivyo.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.