Akaunti ya Instagram ya Wema Sepetu Yarudishwa Baada ya Kushikiliwa Zaidi ya Mwezi.

Kwa muda mrefu msanii wa bongo movie na aliyekuwa mrembo wa Miss Tanzania mwaka 2006  Wema Sepetu ilikuwa imeshikiliwa na watu wasiojulina na hata kubadilisha matumizi ya akaunti hiyo na kumfanya madame Wema Sepetu kutokuwa karibu na mashabiki wake kwa muda mrefu.

Akaunti hiyo ambayo ilichukuliwa na kuanza kutumika kwa baishara ambazo Wema Sepetu hakuwa anazifanya imerudishwa baada ya mafundi na watu wa karibu wa mwanadada huyo kuangaika sana na kufanikiwa kuirudishwa kwake.

download latest music    

Upoteaji wa akaunti hiyo ya Wema Sepetu ulizua ugomvi na uadui kati ya Wema Sepetu na mwanaharakati Mange Kimambi kwa kile kilichodaiwa kuwa Wema Sepetu alikuwa akimtuhumu Mange Kimambi kuwa ndie alikuwa ameshikiria akaunti hiyo.

Akitihibitisha kurudi kwa akaunti yake Wema Sepetu aliposti katika akaunti hiyo na kuandika”alhamudulilah am baaaack…this time for real…thank you Tizzo wangu.”

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.