AKOTHEE- Nahitaji Walinzi Ishirini Kwa Ajili Ya Gari Langu La Thamani

Mwanamama anayefanya vyema Kwenye tasnia ya muziki nchini Kenya Esther au maarufu kwa Jina la usanii kama Akothee ametoa kali ya mwaka kuhusu ulinzi alionao kwake.

Akothee amewaambia mashabiki zake Kupitia mitandao ya kijamii kuwa hivi sasa ana walinzi ‘Bodyguards’ kama ishirini ambao wapo maalumu kwa ajili ya kumlinda kisa gari la thamani analomiliki.

download latest music    

Kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya lakini nane na sabini na Tisa, Akothee ameandika:

Nimeshakuwa maarufu na umaarufu ni mgumu, kwa sasa siwezi kutoka hovyohovyo kama mwanzo kwa sababu watu wengi sasa hivi wananifuatilia.

Maisha yangu yana drama nyingi sana ila mimi sifeki maisha nina gari kubwa na zuri, nina bodigadi kama ishirini hivi na ninawatumia kwa matumizi yangu mbalimbali pia nina watoto wawili Wazungu, watatu Waafrika ingawa siwashawishi waje kuwa na watoto wengi kama mimi“.

Akothee ni mama wa watoto watano na pia ni mfanyabiashara Mwenye mafanikio makubwa sana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.