Ali Kiba Afuta Video Ya ‘Hela’ Youtube Baada Ya Mashabiki Kumvaa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amedaiwa kufuta video ya nyimbo yake ya ‘Hela’ aliyotangaza kuiachia siku ya jana baada ya mashabiki zake kumjia juu.

Ali Kiba  aliachia kazi hiyo usiku wa kuamkia Jumatano hii baada ya kukaa muda mrefu bila kuachia kazi hali ambayo iliwafanya mashabiki wake wachukizwe na kitendo hicho.

download latest music    

Ali Kiba alilazimika kuifuta video ya wimbo wa Hela baada ya mashabiki zake kumgeuka na kumtolea povu zito huku wengine wakidai kwamba wimbo huo ameuridia wimbo wake wa zamani.

Mashabiki walitawala koment na kumchana kuwa wanataka nyimbo mpya kwani hajatoa nyimbo mda mrefu na kipindi ambacho wamekaa wanasubiri nyimbo mpya yeye amefanya video ya wimbo wa miaka ya nyuma.

Baada ya povu hilo Ali Kiba alifuta video ya wimbo huo kutoka Youtube na hajatoa tamko lolote.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.