Ali Kiba Ataja Sababu Za Kutoonekana Uwanjani na Coastal Union

Staa wa muziki wa Bongo fleva aliyegeuka mfanyabiashara na sasa mcheza mpira wa kulipwa kupitia timu ya Coastal Union, Ali Salehe Kiba amefunguka na kutaja sababu za kutoonekana Kwenye mechi yoyote mpaka sasa.

Pamoja na kwamba Ali Kiba alitangazwa kujiunga na kikosi cha Coastal Union Miezi michache iliyopita lakini mpaka sasa Ali Kiba hajaonekana Kwenye mchezo hata mmoja wa timu hiyo.

download latest music    

Ali Kiba amefunguka na kusema kuwa hana haraka ya kucheza kwa sasa na badala yake anausoma mchezo jinsi ambavyo unaenda pamoja na kukosa mechi za Coastal Union dhidi ya Lipuli FC, Biashara United, KMC na African Lyon.

Kwenye mahojiano aliyofanua na Spoti Xtra Ali Kiba amefunguka haya:

Ifahamike kuwa haina haraka ya mimi kucheza kwani mpira una njia na kanuni zake ambazo mtu unatakiwa uzijue”.

Ni lazima uzijue vizuri hizo na siyo unakurupuka na kuingia uwanjani, niko vizuri kabisa ila kwa sasa natafuta kuielewa timu kabla ya kuonekana uwanjani kwenye mechi zijazo za timu yangu”.

Wakati wa usajili wa Kiba, uongozi wa timu hiyo uliweka wazi kuwa Msanii huyo atakuwa huru kufanya shughuli zake za Kimuziki endapo atahitajika kipindi cha mechi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.