Ali kiba, Diamond Wanatumia Ndere-Fredy Makomandoo

Mmoja wa wasanii wa kundi la musiki wa Bongo Fleva nchini  kundi la Makomandoo, Fredy, amefunguka na kusema  kuwa katika miziki wanaoufanya  kuna baadhi ya wasanii wanafanikiwa katika muziki kwa kuboost muziki wao na “ndere” yaani nguvu za giza.Msanii huyo alipoulizwa kuhusu kufanikiwa kwa muziki kuna sababishwa na uchawi alikubali kuwa ndio ni kweli uchawi unahusika na kutaja baadhi ya wasanii, hata hivyo msanii huyo aliambiwa ataje watu watatu lakini akasema kuwa wapo wengi zaidi ya watatu.

“ndere zipo,mi sikatai, mimi mwenyewe natandika ndere” alikiri msanii huyo.Na alipoambiwa ataje wasanii wengine akarudia tena, “mimi mwenyewe ndere,kiba ndere, diamond ndere ‘, alipoulizwa kuhusu kiba akasema “kiba..Alikiba”.

download latest music    

Katika mahojiano na bongo 5 ambapo ndio walipokuwa wanafanyiwa , alikuwepo pia msanii mwingine wa kundi hilo anaejulikana kama muki na yeye alisema kuwa”mafanikio ya mtu yanakuja kutokana na juhudi binafsi, kila mtu kuna jinsi anavyojituma hizo ndo zinaweza kumfanya mtu afanikiwe, lakini ingawa wapo wanaofanya dua na matambiko ..Ila kwa upande wangu huwa ni dua tu, mnaweza kumwita kiongozi wa dini akafanya sala kisha natoa wimbo”alisema Muki.

Wakiwa kama wasanii inawezekana kuna wanachokiona kwa wenzao, na kama kweli kuwa muziki wa Tanzania unafanikiwa kwa sababu ya uchawi basi bado wasanii wanahitaji kufanya jitihada kubwa za kufanikiwa. Wasanii aliowataja ni wasanii wakubwa na wamekuwa pengine mifano kwa wasanii chipukizi katika kutoboza katika sanaa ya  muziki pia.

Makomandoo ni moja ya kundi bora la muziki  ambalo lilianza tangu kipindi cha miaka ya nyuma na wimbo wao uliosikika sana wa’ kibaba baba’ limefanikiwa kukaa kwa muda mrefu katika game bila kuteteleka, yalikuwepo makundi mengi lakini yalishindwa kutunza umoja na kujikuta yanavunjika hii imekuwa tofauti kwa kundi ili ambalo tangu walipoanza  mpaka leo  lakini bado ni kundi la muziki ambalo halina habari za kugombana au kuwa na skendo yoyote mbaya ya kufanya kundi lionekana linafanya vibaya na kwa sasa wanatamba na kibao chao cha “anaona gere”.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.