Alichokiandika Nikki wa Pili Siku ya Mei Mosi Kuhusu Wasanii.

Mwanaharakati na msanii wa bongo fleva Nikki wa Pili amewafumbua macho wasanii wenzake kwa kuwaambia kuwa hakuna haja kwao kusherekea siku ya mei mosi ilhali haina tija kwao kama inavyokuwa na tija kwa wafanyakazi wa serikali.

niki anasema kuwa wasanii wamekuwa wakikosa ulinzi katika maeneo yao ya kazi na hata wakiumia au kufanya kitu chochote siku za kazi hawana pa kwenda kulalamika na kushtaki ili kupatiwa haki zao hivyo badala ya kusherekea siku ya mei mosi ni bora kukaa nyumbani na kuacha kushughulika na mei mosi.

download latest music    

ikiwa leo ni siku ya mei mosi, wasanii haituhusu kwa sababu hatuna ulinzi  wa kisheria wala  wala taratibu tuwapo maeneno ya kazi.hata ukishika mic inashot au steji mbovu  ukaangua au ukavamiwa hakuna pa kukimbilia , hakuna malipo wala fidia yoyote ? hapana kwa sababu halindiw na shrria ya kazi hawapo mahali pa kazi.ndugu msanii pambana na hali yako  na ulinde maadili ya kazi.

Niki amekuwa akitoa nasaha nyingi sana kwa vijana huku akiamini kuwa kuajiriwa ni kama kuwa mtumwa, ni bora kujiajiri na kuwa bosi mwenyewe.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.