Alichokiongea Dudubaya Kuhusu BASATA na Wasanii Kufungiwa

Msanii wa bongo fleva Dudubaya amefunguka na kusema kuwa amekuwa akikerwa na tabia ya baraza la sanaa kwa wanawafungia wasanii kazi zao kwa sababu za kuvuja maadili .Kwa kitendo hicho Dudubaya amekiita ni ukurupukaji kwa sababu wanafanya vitu hivyo  bila  kuwa na muongozo maalumu.

Hata hivyo Dudubaya anasema kuwa inakuwa haina maana kuufungia wimbo ambao tayari ulishasambaa katika mitandao na kwenye simu za watu hivyo inakuwa haina maana ya kuufumgia kwa sabau watu nwalishauona.dudubaya anasema kuwa kitendo wanachofanya ni kukurupuka na kufuata mihemuko ya mashabiki lakini lengo lao sio kurekebisha maadili.

download latest music    

Lakini pia Dudubaya alisema kuwa kama BASATA wanataka kufanya lengo lao liweze kufanikiwa ni lazima waweke mkakati wa kufanikisha hilo kwa kuandaa blog ambayo itabidi kazi zote za sanaa zitapitia hapo kabla ya kutolewa kwa mashabiki wao.

Nampongeza sana naibu waizri kuwa nafanya jitihada katika kukuza na kufanya tasnia ikiue lakini pia kutunza maadili ya wasanii,lakini nimekuwa nikikerwa sana na swala la kufungiwa kwa wasanii hasa audio na video za wasanii kwa sababu hazina maadili wakati tayari zilishatapakaa mitaani na katika simu za watu.wanachofanya ni kukurupuka tu kama mtu aliyekuwa amezama kwenye maji.

Dudu baya anasema kuwa watakapo anzisha blog wa ajili ya kuweka nyimbo na audio za wasanii itakuwa ni vizuri na itasaidia kutangaza kazi za wasanii kwa sababu kila wimbo utakapitia hapo na wao watakuwa ndio watu wa mwisho kutoa go-ahead kuwa nyimbo hiyo ipo sawa na imekaguliwa na kuthibitishwa kuwa inafaa kusikilizwa na watu, akitolea mfano anasema kuwa mbona vyakula vinakaguliwa na TFDA.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.