Alichokiongea Mad Ice Kuhusu Harmorapa

Mwanamuziki wa Ragger na Bongo Fanaefanya kazi zake nchini Tanzania na Uganda pia  Ahmed  Mohamed Kakoyi maarufu kama Mad Ice  amefunguka na kuongelea kipaji cha muziki alichonacho Harmorapa na kazi anayoifanya kwa ujumla,msanii huyo ambae ni raia wa Uganda lakini amekuwa akifanya vizuri nchini Tanzania katika muziki anasema kuwa msanii Harmorapa afai kabisa kuitwa msanii wa Bongo Fleva maana hana kipaji cha Bongo Fleva na wanaompa sifa hizo ni kama wanaua sanaa ya muziki wa bongo.

Alipokuwa akizungumza na kituo cha East Africa Radio katika kipindi cha Planet Bongo, Mad Ice alisema kuwa kipaji chake kinafaa kuwa ni uchekeshaji,”nimesikia ilo jina la Harmorapa nikasikitika sana,kwa sababu kuna vitu tunafanya vinaharibu sanaa yetu wenyewe, kuna baadhi ya wasanii  wanahitaji kupewa fursa, mimi nimemuona kama mchekeshaji tu ,ukiniambia ni comedian nitaheshimu lakini  unaponiambia unamlinganisha na mimi  nitakuona una kitu kinakusumbua kichwani‘ amefunguka Mad Ice

download latest music    

Hata hivyo sio mara ya kwanza kwa wasanii wakongwe kama Mad Ice kutoa kauli kama izo zinazomuhusu Harmorapa, msanii aliyekuja na kuchukua jina katika tasnia ya musiki kwa muda mfupi kutokana na mambo na vituko vyake alivyokuwa akifanya huku wengine wakimshtumu kuwa anatafuta kiki, Harmorapa aliingia katika bifu na baadhi ya wasanii wakubwa kipindi anaanza musiki.Hata hivyo kwa sasa msanii huyo anaonekana kupoa kabisa zile kiki zilizokuwepo mwanzo zimekuwa kimya.Producer maarufu nchini, Master J pia alishawahi kutoa maoni yake juu ya Harmorapa na kauli yake haikupishana na  hii ya Mad Ice kuwa Harmorapa alifaa kuwa msanii wa vichekesho lakini sio Bongo Fleva .

Akiwa kama msanii mkongwe Mad Ice aliyefanikiwa sana kimuziki , alipoanza kufanya kazi chini ya Mikka Mwamba na alifikia hatua ya kutangaza nyimbo zake mpaka katika soko la muziki la Ulaya na kutokana na kujituma kwake na kufanya vizuri katika nyimbo zake mbalimbali msanii huyo alipata bahati ya kualikwa mara nyingi katika matamasha nchini Ulaya ,kitu ambacho kilimfanya muziki wake uendelee kukua.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.