Alichosema Man Walter Kuhusu Kolabo ya Daimond na Alikiba.

Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva, Man Walter amezungumza kwa ufupi endapo itatokea siku moja  msanii Diamond na Alikiba wanaweza kufanya kolabo ya pamoja , hata hivyo Man Walter ambae amekuwa akifanya kazi na watu hawa wawili anasema kuwa hajawahi kusikia kitu hicho kutoka kwa wasanii hawa wenyewe ingawa amekuwa akikutana nalo sana swali hilo.

Mimi sijawahi kusikia kama kuna plan,alafu hilo ni swali ambalo nimekuwa nikiulizwa zaidi ya mara mbli au mara tatu kwangu hata sijui kwanini hivyo,hawa watu wana management, wana mambo yao kwahiyo hata sijui chochote.

labda kama kuna mtu anataka kuomba msada wa kuwshawishi hawa vijana kwa sababu ni wadogo zangu na ni ndugu zangu wote nilishawahi kufanya nao kazi.

Hata hivyo man walter anasema kwamba kama wawili hao wanafanya hivyo kama kazi na baishara basi waendelee kufanya lakini sio kufanya kwa chuki .

download latest music    

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.