Alikiba Awataka Mashabiki Wake wa Mpira Kumsubiri Tanga.

Msanii wa muziki wa bongo fleva amefunguka jana alipokuwa katika sherehe ya mdogo wake ambapo jana zabibu kiba alipofanya sherehe ya harusi yake alipoolewa na mchezaji wa timu ya taifa.

Alikiba ambae aliwaacha mashabiki wake wengi katika wakati mgumu baada ya kusajiriwa na timu ya coastal union hivyo mashabiki wake kuapata wasiwasi ni jinsi gani anaweza kujigawa kufanya muziki na kucheza mpira uwanjani.

download latest music    

Akiongea na mc pilipili ambae alikuwa MC katika harusi hiyo, alikiba alipoulizwa alisema kuwa majibu ya maswali yao yote watayapata siku ya mpira.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wake na watu wa karibu  wamemuelewa msanii huyo huku wakisema kuwa alikiba hawezi kuongea chochote kwa sasa kwa sababu mamlaka hayo yameachwa katika uongozi wake  wa timu.

Hata hivyo uongozi wa Coastal Union walisema kuwa pamoja na kwamba wamefanya usajili na alikiba lakini inapotokea alikba anataka kufanya kazi zake za muziki wako tayari kumruhusu kuendelea na kazi.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.