“Alikuwa na pesa nyingi, lakini ameshindwa kununua uhai” Waigizaji wa Bongo Movie waongea matope kuhusu kifo cha Ivan

Tofauti na wasanii wengine ambao walitoa salamu za rambirambi kufwatia kifo cha Ivan Ssemwanga, Steve Nyerere and Faiza Ally wameeleza hisia kali kuhusu kifo cha aliyekuwa mume wa Zari.

Waigizaji hao wa Bongo Movies wameongea matope kuhusu kifo cha Ivan, hisia zao kuhusu kifo cha mwenda zake zinaonyesha uadui tu.

download latest music    

“Alikuwa na pesa nyingi, alikuwa na uwezo wa kufanya chochote, alikuwa na uwezo wa kununua chochote lakini ameshindwa kununua uhai. Nimejifunza kitu kupitia wewe, tuishi vizuri na watu maana hakuna ajuaye kesho,” Steve Nyerere aliandika.

Steve Nyerere

“Binaadamu akikuchukia hata zuri kwake ni baya na ndio maana huwa na maisha yangu tu kama mimi bila kutaka kuwa yoyote, hakuna zuri mbele ya mtu mbaya. Unajua nini wala sijali naona upuuzi tu kama ya kipuuzi mengine yote yalio pita.

“Maisha yangu na wanangu yako kwenye mikono salama hata kushinda mikono yangu, yako kwenye mikono ya Mungu mwingi wa rehma. Leo Ivan na matajiri wengine wako wapi? Mali sio kila kitu kwenye maisha yetu tunahitaji amani, mapenzi, maelewano makubaliano.

Faiza Ally

“Nimetoka kwenye kutokua na mlo mpaka sasa namiliki milo, huo ni utajiri mkubwa maana kwanza ni kushiba akili ikae sawa ndio upange habari zingine, so at the end my heart is pure and that what give me amani ya moyo, hayo mengineyo tena yako nje ya uwezo wangu ni mipango ya Mungu, Faiza Ally aliandika.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere