Amber Lulu aacha mambo ya kuuza sura kwa video za wasanii wa Bongo

Amber Lulu ni mmoja wa warembo ambao wanatajika sana kwa kuuza sura (video vixen) kwenye video za wanamuziki wa Bongo.

Lulu ametokea kwenye video nyingi kama ile ya ya Dully Sykes na Harmonize ‘Inde’ na zingine. Mrembo huyo sasa hataki mambo ya kuuza sura kwa video za wasanii wa Bongo.

download latest music    

Akiongea na E-Newz ya EATV, Amber Lulu alisema kuwa ameanza kuimba na hataki kufanya mambo ya video vixen kwani itakuwa kama kupiga hatua nyuma.

 

“Sasa hivi nafanya muziki sio video vixen tena kwa sababu nimeshaingia kwenye muziki kwa hiyo nikifanya video vixen nakua kama narudi nyuma na mimi sitaki kurudi nyuma tena nahitaji nifanye vitu vipya. Inatakiwa kama ni muziki wangu niufanye wa international au nizidishe sitaki kurudishana nyuma.

“Maoni niliyoyapokea kwa watu wengi ni mazuri sana, wengi wananishauri vitu vingi kuhusu muziki, kuna baadhi ya wasanii kama wakina Shilole na Chege nimeshakaa nao kuna vitu wameniambia unatakiwa ufanye,” amesisitiza Amber Lulu,” alisema Amber Lulu.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere