Amber Lulu aeleza sababu hawezi toka kimapenzi na wanamuziki wa Bongo

Amber Lulu anaonekana kuwa anazifuata nyayo za Gigy Money kwani pia yeye anajitambulisha kama muimbaji. Video vixen huyo kutoka Tanzania hata hivyo amefunguka kueleza sababu yeye Kama mwanamke hawezi taka kutoka kimapenzi na wasanii wa Bongo.

Amber Lulu alibainisha haya alipokuwa akizungumza na Bongo Dot Home ya Time Fm akisema kuwa wasanii wengi wa Bongo hues hawana msimamo na kwa sababu ya jambo Kama hilo, yeye hatamani kupata mpenzi anayefanya mziki wala mtu maarufu. Amber Lulu alisema,

download latest music    

” Mastaa wengi bongo ni wasumbufu sana, mimi huko nyuma niliwahi kuwa katika mahusianio na hao mastaa nikaona aah basi bora niachane nao, naona walivyo kwa sasa na najua wanavyoishi ndio mana sina mpango nao.”

Aliendelea kwa kusema,

“Wastaa wengi hawako serious sana na hata kwenye maisha yao hawako serious, mie naona mastaa naoshindanao naona kabisa hata akiwa na mpenzi kuna kitu kinamiss , unakuta mtu anakaa na watu hata watano yani.”

 

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua