Amber Lulu Amuanika Mpenzi Wake Mpya Baada ya Kumwagana na Prezzo

Video vixen na msanii wa Bongo fleva, Lulu Eugene maarufu kama Amber Lulu amemuanika live mpenzi wake mpya baada ya kumwagana na staa wa muziki kutoka Kenya, Prezzo.

Prezzo na Amber Lulu walikuwa kwenye mahusiano  kwa miezi kadhaa ambapo mara kwa mara pamoja na penzi lao kupondwa na watu kadhaa ikiwemo kama msanii TID, lakini walisisitiza penzi lao ni la kweli na litadumu.

download latest music    

Lakini baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kupostiana Kwenye mitandao ya kijamii tetesi zilianza kusambaa kuwa wawili hao wameachana ingawa hakuna aliyethibitisha hilo mpaka wikiendi iliyopita kwenye birthday party ya Amber Lulu.

Global Publishers wanaripoti kuwa siku ya Jumamosi Amber Lulu alifanya party ya birthday ambapo alialika watu kadhaa na moja kati ya wageni alimtambulisha mwanaume mmmoja kama Sam ambaye aliweka wazi kuwa ni mpenzi wake.

Amber Lulu na Mpenzi Wake Sam

Amber Lulu alimtambulisha mpenzi wake Sam kwa wageni waliohudhuria sherehe hiyo na kusema:

Jamani huyu ndio naniliuu wangu yeye ni mkurugenzi hapa mjini lakini sitaki kumpamba sana kwenye pati yangu hii nisije nikaibiwa buree na vidaka tonge vya mjini, naomba kwa leo mjue hivyo tu”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.