Amber Lulu Apewa Kichapo Cha Mbwa Koko na Young Dee

Video Vixen na msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na Single yake ya ‘Jini kisirani’ Lulu Euggen maarufu kama Amber Lulu amekiri kupokea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa msanii mwenzake Young Dee.

Wiki iliyopita kipindi cha XXL cha Clouds Fm waliripoti kuwa Kwenye studio fulani hapa Mjini Amber Lulu alionekana akiwa anapigwa vibao, ngumi na hadi mateke na Young Dee.

download latest music    

Baada ya kipigo hiko Amber aliweka wazi kuwa sababu iliyomfanya mpaka Young Dee ampige ni baada ya kukataa kuwa naye Kimapenzi na kisha kutinga ndani ya studio hizo na mwanaume mwingine.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Amber alikiri kupigwa na Young Dee lakini amesisitiza kuwa ulikuwa ni wivu wa kimapenzi:

Kweli Young Dee amenipiga kwa ajili ya wivu mimi ni mzuri lazima unitamani we mwenyewe umeona hili tak* usilitake Tena ? Mimi ni mzuri alafu ananitaka halafu mimi simtaki siwezi kuwa na bwana mariooo alivyoniona akaanza kuniletea Sholo nyingi alafu mimi sitaki shobo”.

Amber Lulu ameshawahi kuwa na Mahusiano na Young Dee katika siku za nyuma lakini wawili hao walishaachana ingawa Amber amekiri mara kwa mara kuwa anampenda sana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.