Amber Lulu- Aslay Ameshawahi Kufaidi Penzi La Wema Sepetu

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Jini Kisirani’ Amber Lulu amefunguka na kupasua kuwa Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameshawahi kufaidi penzi la staa wa Bongo fleva Aslay.

Amber Lulu, ametoboa siri ya Wema Sepetu na Aslay kuwa wapenzi miaka ya nyuma lakini pia amedai waliwahi kuishi pamoja kinyumba kama mke na mume.

download latest music    

Wiki iliyopita Amber Lulu alianika hadharani kuwa yeye na Aslay walishawahi kuwa Kwenye Mahusiano pale alipoanika orodha ya wanaume ambao ameshawahi kubanjuka nao.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Amber Lulu ameweka wazi kuwa kipindi alipokuwa na Aslay alisikia pia alikuwa na Wema Sepetu aliyekuwa anaishi naye nyumba moja kitendo kilichofanya Mahusiano yao yasiwe serious:

Kipindi hiko nilikuwa undergrad nikawa nasikia Aslay alishakuwa na watu wengi nasikia alishakuwa na Wema Sepetu na wakakaa nyumba moja na wakapika na  kupakua halafu mimi kipindi hiko bado kabisa nilikuwa nanyapia nyapia”.

Amber Lulu amedai kuwa Aslay alikuwa ni fundi mzuri sana kunako mausuala ya sita kwa sita huku pia akitumia sifa hiyo kumtofautisha na Mbongo Fleva mwingini, Young D ambaye nae pia alikuwa mpenzi wake lakini hakuwa fundi sana kama ilivyo kwa Aslay.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.