Amber Lulu Aweka Mapenzi Pembeni Baada Ya Kuumizwa

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Jini kisirani’ Lulu Euggen maarufu kama Amber Lulu amedai ameamua kuweka masuala ya mapenzi pembeni.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Amber Lulu ameweka wazi kuwa, amekuwa kwenye mahusiano mengi, lakini anaona ni kama anapoteza tu muda wake tu.

download latest music    

Mapenzi yameninyoosha bora niyapige chini maana wanaume wengi wananipenda kwa sababu ya umaarufu wangu, lakini unakuta hawana mapenzi ya kweli kwangu. Ninaona tu huko ninapoteza muda na kuambulia maumivu, kwa hiyo bora nijiweke wazi tu, hakuna namna“.

Amber Lulu amemaliza Mahusiano Yake ya kimapenzi siku chache zilizopita na Msanii kutoka +254 Nairobi, Kenya Kwa tuhuma za kuzidisha michepuko.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.