Amber Lulu: Hakuna Kilichotokea Kati yangu na Prezzo

Image: Amber Lulu

Video vixen maarufu mtandaoni Amber Lulu amefungukia ishu yake na Mwanamuziki wa Kenya Prezzo na kudai kuwa hakuna chochote kilichotokea baina yao.

Amber Lulu aliongea hayo baada ya tetesi kusambaa wiki chache zilizopita baada picha za wawili hao kusambaa mtandaoni huku zikiwaonyesha wakiwa katika mikao ya kimahaba na kuleta gumzo na hata kuonekana hotelini pamoja.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na East Africa tv katika kipindi cha Friday night live Amber Lulu alifunguka kuwa hakuna kitu chochote kilichotokea baina yao hasa upande wa uhusiano wa kimapenzi.

“Watu wengine washamba lakini ni vitu fulani vya kinyamwezi tu ambapo unaweza kukaa chumba kimoja lakini msifanye kitu chochote, unajua ndege wawili wanaofanana huwa wanaruka kwa pamoja kwaiyo Prezzo ni Kama rafiki kwangu hivyo hakuna tatizo la sisi kuwa hivi tulivyo”.

Pia Amber Lulu alimalizia kwa kudai kuwa watu walizusha kuwa yeye na Prezzo walionekana hotelini pamoja kitu ambacho sio cha kweli kwani walikaa kwenye nyumba ambayo ni apartment ambapo kila mmoja alikuwa na chumba chake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.