Amber Lulu- Ma-video Queen Wa Kibongo Hawana Hela Wanajua Kudanga Tu

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha Jini Kisirani Amber Lulu amefunguka na kuweka wazi kuwa mavideo Queen wa kibongo hawalipwi vizuri wanategemea kudanga tu.

Amber Lulu alijizolea umaarufu kutokana na kuwa video queen ambazo ameshaonekana Kwenye video za Wasanii kibao.

download latest music    

Baadaye Amber Lulu aligeukia muziki wa Bongo fleva ambao umekuja kumpa mafanikio Kupitia kibao chake cha jini kisirani.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv,  Amber Lulu anafunguka na kuweka wazi kuwa wasichana ambao wanatumika kama mavideo Queen Kwenye video za wasanii hawana pesa na hawalipwi vizuri hivyo wanaishia kudanga.

Kusema kweli kibongo Bongo bado uvideo vixen haulipi wengi wanakuwa wanadanga tu na labda uwe unafanya biashara nyingine extra lakini u-video vixen haulipi we mtu unakaa gheto kali lakini unavaa Brazilian hair, unashika simu kali alafu unasema unalipa nani anakulipa? Utaishia kupanda vibajaji hata uber hupandi”.

Lakini pia Amber Lulu amefunguka kuwa muziki unalipa sana mtu unaweza ukaendesha maisha yako kupitia muziki.

muziki unalipa unaweza ukafanya kila na kuendesha maisha yako kila kitu na hata kulipa bili mbali mbali “.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.